July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFDA yaeleza mafanikio ndani ya miaka 10

Spread the love

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema imeimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa mbalimbali katika miaka 10 ya serikali ya awamu ya nne. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam walipowasilisha mafanikio yao waliyoyapata ndani ya Serikali ya awamu ya nne 2005-2015.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa TFDA, Gaudensia Simwanza amesema kuimarishwa kwa mifumo ya udhibiti kumeongeza kasi ya usajili wa bidhaa, ukaguzi wa maeneo ya biashara, upimaji wa sampuli kimaabara na ufuatiliaji wa ubora sokoni.

Simwanza amesema idadi ya bidhaa zilizosajiliwa zimekuwa zikiongezeka kila mwaka kutoka 2,357 mwaka 2005 hadi kufikia 7,062 mwaka huu, ambapo viwanda 7,877 kati ya 7,938 vya uzalishaji bidhaa vilivyopo ndani na nje ya nchi vilikaguliwa na kukidhi vigezo na bidhaa zake kuruhusiwa kuingia nchini.

Ameongeza, TFDA imeboresha udhibiti wa bidhaa katika vituo rasmi vya forodha 32 kwa kuweka wakaguzi na vifaa vya ukaguzi ikiwa ni pamoja na maabara ndogo zinazohamishika (mini-lab kits) kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali wa bidhaa kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini.

Pia Simwanza amesema kukamilika kwa jengo la Makao Makuu ya TFDA la kuhifadhi kumbukumbu ambapo lilikamilika mwaka 2009 pamoja na upanuzi wa maabara yao kutoka ghorofa moja hadi mbili na kuongeza vifaa vya uchunguzi ni moja ya mafanikio yaliyoweka mazingira mazuri ya ufanyaji kazi na ufanisi mkubwa wa kiuchunguzi.

Simwanza amesema wamefanikiwa kuifanya maabara ya mamlaka hiyo kuwa na viwango vya kimataifa vya umahiri wa uchunguzi ambapo maabara ya dawa imesajiliwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (WHO) baada ya kufanya majibu ya uchunguzi kutambuliwa kimataifa, maabara hiyo imepewa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005.

Hata hivyo Simwanza amesema wamefanikiwa kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa za msingi katika maeneo ya vijijini na miji midogo, kwa ambapo jumla ya maduka 4,041 yamefunguliwa, pia watoa dawa 13,023 na wamiliki 11,872 walipatiwa mafunzo.

Aidha amesema katika kuimarisha usimamizi wa Rasilimali mamlaka imeendelea kuajiri watumishi ili kuongeza nguvu katika shughuli za udhibiti, idadi ya watumishi imeongezeka kutoka 85 Juni 2005 hadi 237 Juni mwaka huu.

error: Content is protected !!