September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tetemeko la ardhi latikisa Dodoma

Spread the love

TETEMEKO la ardhi katika Mkoa wa Dodoma limetokea saa 12: 01 asubuhi na kutishia maisha ya wakazi wa mji huo, anaandika Dany Tibason.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Swaswa, Kata ya Ipagala Manispaa ya Dodoma wamejikuta katika wakati mgumu huku wengine wakikimbiza watoto wao baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.

Tukio hilo limewafanya baadhi ya wakazi hao kukimbia makazi yao na wengine kuwakimbiza watoto wao kutoka ndani ya nyumba kwa hofu ya kuangukiwa na nyumba. Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa Richter Scale 5.1.

Kutokana na tukio hilo, baadhi ya wazazi walipatwa na mshutuko huku watoto wakiangua kilio kutokana na mtikisiko wa tetemeko la ardhi.

Watanzania wametaadharishwa kutokimbia ovyo pale yanapotokea matetemeko makubwa ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.

Taadhali hiyo ilitolewa leo na Gabliel Mbogoni, Ofisa Giolojia Mwandamizi wa Wakala wa Giologia nchini alipozungumza na waandishi wa habari juu ya kutokea kwa tetemeko lililotokea.

Amesema eneo la Aneti lipo katika Ukanda wa Bonde la Ufa Mkondo wa Mashariki na kwa upande wa Mashariki wa Aneti kuna matukio mengi ya matetemeko na kwamba, eneo la Ziwa Natroni kuna Mlima wa Volkano ambao mpaka sasa unafukuta.

Amesema, madhara ya matetemeko yanategemeana kwani yanaweza kuwa makubwa au yasiwe na madhara na kwamba, kiwango cha tetemeko la leo lenye ukubwa wa Richter Scale 5.1 ni kubwa linaweza kusababisha uharibifu wa kubomoka kwa nyumba au uharibifu wa miundombinu.

Mbogoni amesema, “kwa tetemeko lililotokea Aneti ni kubwa kwa kutokea katika Mji wa Dodoma kwani tetemeko kubwa ambalo liliwahi kutokea, lilikuwa la Mlima Olidonyolengai ambalo lilikuwa na ukubwa wa Richter Scale 5.9 mwaka 2007.”

Hata hivyo amesema, licha ya kuwa tetemeko hilo liliweza kufika katika Mikoa ya Tanga, Arusha, Dar es Salaam na mikoa jirani, hawajapata taarifa yoyote ya kutokea kwa madhara.

error: Content is protected !!