January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Temeke: Tumedhibiti kipindupindu

Spread the love

HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam imefanikiwa kudhibiti maambukizi -mapya ya ugonjwa wa kipindupindu ambapo hakuna mgonjwa ndani ya wiki mbili mpaka sasa. Anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na MwanaHALISI Online jijini Dar es Salaam leo, Joyce Msumba, Ofisa Uhusiano Manispaa ya Temeke amesema kuwa, tangu tarehe 13 Januari mwaka huu mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya kuwepo kwa wagonjwa wapya.

“Tangu tarehe 13 Januari hadi sasa, Mganga Mkuu wa Manispaa hajapokea taarifa za uwepo wa wagonjwa wapya wa kipindupindu au vifo kwenye
kambi zetu za Hospitali ya Temeke na Kigamboni,” amesema Msumba.
Msumba amedai kuwa, tangu ugonjwa huo ulipuke wagonjwa 816 walidhaniwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu lakini baada ya kufanyiwa vipimo,
iligundulika 205 walipata maambukizi, kati yao 16 wamefariki dunia.
“Manispaa ilijitahidi kutoa elimu na dawa za kuuwa wadudu kama Chlorine ambazo zilikuwa zinamwagwa kwenye vyoo na visima na dawa za
kutibu maji (Water guard),” amesema.
amesema, takribani kaya 100 kati ya kaya 23,091 zilipata huduma ya usafi wa mazingira yao, vyoo vya kaya 100 vilitibiwa kwa dawa za kuua wadudu pia visima vifupi ambavyo vilipimwa na kubainika vimeathirika na vinyesi, vilifukiwa  ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo.

“Manispaa kwa kushirikiana na mabwana afya, watendaji wa mitaa na watumishi wa afya, walizunguka Temeke nzima ili kuhakikisha mazingira
yanakuwa safi ikiwemo usafi wa mitaro isiyotiririsha maji,” amesema na kuongeza;

“Manispaa imeandaa operesheni maalum ya kupita mitaani ili kuangalia wito wa wananchi kufanya usafi na ikibainika kuwepo kwa mkazi anayechafua
mazingira kwa kusudi hasa kufungilia majitaka na kuyaelekeza kwenye mitaro, atachukuliwa hatua za kisheria.”amesema.

error: Content is protected !!