January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TEMCO: Uchaguzi Z’bar ulikuwa huru

Spread the love

TAASISI inayojishughulisha na uchaguzi nchini (TEMCO) imesema, uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika kwa uhuru na haki kinyume na taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TEMCO, Dk. Benson Banna amesema “TEMCO ilipokea kwa mshtuko na mshangao uamuzi wa kufuta matokeo ya uchaguzi uliotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.

Wiki iliyopita, wakati ZEC ikiendelea kuhesabu kura, Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kwa kile alichoeleza kuwa “ukiukwaji na uvunjaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.”

Mifano iliyonukuliwa na Jecha katika kuhalalisha kufuta uchaguzi huo ni vitisho kwa wapiga kura hasa kwenye maeneo ambako ni ngome za vyama, kupoka mamlaka ya tume juu ya utangazaji matokeo ya kura ya urais, idadi ya wapiga kura katika vituo kuzidi ile ya waliojiandikisha hasa pemba na wajumbe wa tume kupigana.

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa shughuli zote za kabla ya uchaguzi zilifanyika kwa weledi na kwa misingi ya sheria, kanuni na taratibu kwa amani na utulivu. Inashangaza kwa uamuzi wa kusitisha uchaguzi uliotolewa wakati tayari kura zikiendelea kuhesabiwa na matokeo kutangazwa,” amesema Dk. Banna.

Amesema kulikuwa na waangalizi wa uchaguzi 22 wa muda mrefu na 704 wa muda mfupi wa TEMCO huko Zanzibar. Waangalizi wa uchaguzi wa muda mrefu waliwasili Zanzibar siku 43 kabla ya uchaguzi.

Kwa pamoja waliangalia michakato ya uchaguzi ikiwemo siku kupiga kura, kuhesabu kura, kutangza matokeo na yaliyojiri mara tu baada ya matokeo kutangazwa.

error: Content is protected !!