July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Teleza Kidigitali ya NMB yatua Kahama, Wamachinga waipokea

Spread the love

PROMOSHENI ya teleza kidigitali ya Benki ya NMB nchini Tanzania imeendelea kusambaa nchini humo kwa kufika Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Meneja wa NMB kanda ya Magharibi Sospeter Magesse, akizungumza na wamachinga juu ya huduma mbalimbali za Benki ya NMB baada ya kuzindua promosheni ya teleza Kidigitali kwenye stendi ya mabasi CDT katika Halmashauri ya manispaa ya Kahama. Promosheni ya teleza kidigitali imelenga kutoa elimu kwa wateja na watanzania kwa ujumla juu ya huduma za Benki ya NMB kama Mshikofasta, NMB pesa wakala na Lipa mkononi

Promosheni hiyo imezinduliwa leo Jumatatu, tarehe 13 Juni 2022 na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magesse.

Sospeter amezungumza na watu mbalimbali wakiwemo wamachinga kwenye stendi ya mabasi CDT juu ya huduma mbalimbali za NMB kuhusu promosheni hiyo.

Promosheni ya teleza kidigitali imelenga kutoa elimu kwa wateja na Watanzania kwa ujumla juu ya huduma za Benki ya NMB kama Mshikofasta, NMB pesa wakala na Lipa mkononi.

error: Content is protected !!