Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TEF yataja tamu, chungu muswada sheria ya habari
Habari Mchanganyiko

TEF yataja tamu, chungu muswada sheria ya habari

Deudatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)
Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limesema limeunda kamati ndogo ya watu sita, kwa ajili ya kuchambua Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, uliowasilishwa bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameleezwa jana tarehe 17 Februari 2023 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, akizungumza katika kipindi cha Kipima Joto, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, ambacho kilikuwa kinajadili kama muswada huo una tija kwa waandishi wa habari.

Balile alisema kuwa, mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa habari kuhusu marekebisho vifungu kandamizi vya sheria hiyo, baadhi yamefanyiwa kazi na mengine yameachwa.

“Si yote yaliyopita ambayo tumependekeza, lakini si yote yaliyobaki. Yaani kuna mabadiliko makubwa yaliyotokea,” alisema Balile.

Mwenyekiti huyo wa TEF, alitaja baadhi ya mapendekezo ya wadau yaliyopita katika muswada huo, ikiwemo makosa yanayotokea katika tasnia ya habari kutokuwa kesi ya jinai.

“Kuhusu suala la criminal defamation tumelia kwa muda mrefu sana kwa maana kwamba wewe umetoa kauli badala ya mhusika kwenda mahakamani kulalamika unashtakiwa na Serikali. Miaka iliyopita watu walipelekwa sana Kisutu umemtukana waziri,” alisema Balile.

Balile alisema “sasa waziri ni Mtanzania kama Balile, waziri akisemwa katika masuala yanayomhusu yeye anapaswa yeye aende afungue kesi ya jinai. Katika mapendekezo yaliyoingia bungeni kwenye kifungu cha 50 (1) na cha 50 (c), wameondoa hili.”

Balile alisema pendekezo lingine ambalo limepenya katika muswada huo, ni kuondolewa kwa kifungu kinachompa mamlaka Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, kuratibu matangazo ya Serikali yanayokwenda katika vyombo vya habari.

Mdau huyo wa habari alisema mapendekezo mengine yaliyofanyiwa kazi ni kuondolewa kwa kifungu cha 38 (3), ambacho kilikuwa kinafuta haki ya kinga kwa mwanahabari anayechapisha habari zilizopewa kinga.

“Kingine ambacho tunaishukuru Serikali ni katika kifungu cha 38 (3) kilikuwa kama kuna habari ambazo zimepewa kinga kwamba ikitokea bungeni na mahakamani, sheria imeweka vifungu kuanzia 38 (1) A mpaka B ilikuwa inasema kwamba habari zote zitakazotangazwa mwanahabari hautawajibika,” alisema Balile.

Balile alitaja pendekezo lingine lililofanyiwa kazi, ambalo ni kuondolewa kwa kifungu cha 50 (4,5,7), kilichokuwa kinaelekeza kutaifishwa kwa mtambo unaochapisha habari za uchochezi na kashfa.

Aidha, Balile alitaja baadhi ya mapendekezo ambayo yamechwa katika muswada huo, ikiwemo uondolewaji wa kifungu kinachoipa Serikali mamlaka ya kulazimisha vyombo vya habari binafsi kutangaza habari kwa wakati fulani.

“Kifungu cha 9 (A na B), kinampa mamlaka mkurugenzi wa idara ya habari maelezo kuwa mlalamikaji, mwendesha mashtka na mtoa hukumu. Katika suala linalohusiana na leseni hoja yetu tuondoke katika utoaji leseni twende kwenye usajili kama zamani,” alisema Balile na kuongeza:

“Sababu wamekataa kuondoa leseni, tutunge kanuni mbadala ya kutompa mamlaka ya moja kwa moja anapaswa kuwa chini ya kanuni itakayomlazimu kuwa na kamati itakayompa ushauri na mapendekezo atakayopaswa kufanya anapotaka kufuta, kunyima au kusitisha leseni.”

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe, alisema kwa kuwa muswada huo umesomwa kwa mara ya kwanza, bado nafasi ya wadau kuwasilisha maoni kwa ajili ya kuurekebisha ipo.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe

Naye Mjumbe wa Umoja wa Wadau wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), Deus Kibamba, amewataka wadau wa habari kuendelea kupaza sauti ili mapendekezo yaliyosaliwa yafanyiwe kazi bungeni.

“Nadhani Bunge liko kwa ajili ya kutunga sheria, leo Serikali imepeleka mapendekezo bungeni na haiwezekani lisibadili chochote. Muswada huu ulivyo huku kwa wadau kukiwa kimya kusiwe na malalamiko yoyote Bunge litapitisha hivyo hivyo, lakini kukiwa na malalamiko utarekebishwa,” alisema Kibamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!