Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa TEF yamwangukia Rais Samia muswada wa habari kukwama kuwasilishwa bungeni
Habari za Siasa

TEF yamwangukia Rais Samia muswada wa habari kukwama kuwasilishwa bungeni

Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)
Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aingilie kati ili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, uwasilishwe bungeni kwa ajili kupatikana sheria bora isiyokandamiza uhuru wa tasnia hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 8 Februari 2023 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, ikiwa ni siku moja tangu Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kusema muswada huo umeshindwa kuwasilishwa bungeni katika vikao vya mhimili huo vinavyoendelea hivi sasa, kutokana na kukosekana kwa nafasi.

“Kwa kuwa Juni 2021 Rais Samia alielekeza TEF na wadau tukakae na Wizara inayosimamia habari tuzungumze jinsi ya kubadili sheria hii ili ikidhi viwango vya kimataifa na kwa kuwa alisema tukikwama sehemu yoyote au tukashindwa kuelewana tusisite kurudi kwake,”

“ Basi tunaomba atupe nafasi ya kukutana naye tumweleze wapi tumekwama na wanaokwamisha ni kina nani, pengine akiwauliza yeye watampa majibu ya msingi kuliko tunavyoshuhudia wakitupuuza sisi kwenye vikao,” imesema taarifa ya Balile.

Akizungumzia sababu zilizotolewa na Msigwa zilizopelekea muswada huo kukwama, Balile amedai kwamba ni nyepesi na inayowapa wasiwasi wadau wa habari iwapo kuna utashi wa kufanywa mabadiliko katika sheria hiyo.

Mwenyekiti huyo wa TEF amesema kwamba, wadau wa habari walipata matumaini baada ya Waziri anayesimamia tasnia hiyo, Nape Nnauye, kuahidi kwamba muswada huo utawasilishwa bungeni Februari mwaka huu, baada ya mapendekezo yao kuwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Kwa namna ya ajabu, muswada huu umeshindikana kuingia bungeni tena (Februari, 2023). Tunajiuliza kama taarifa za kamati zimezuia muswada kuingia bungeni, je, muswada huu utapataje nafasi kwenye mkutano ujao wa Aprili, 2023? Je, itawezekana vipi katikati ya hotuba za Bunge la Bajeti la mwaka 2023/2024?” amehoji Balile.

Balile amesema kuwa, TEF inasikitishwa na kitendo cha marekebisho ya sheria hiyo kuchukua muda mrefu, kwa kuwa haki ya uhuru wa habari siyo ya wanahabari peke yake, bali ni uhuru wa watanzania wote kutoa maoni yao, kitendo kitakachokuza demokrasia nchini na kuongeza uwajibikaji.

Hii ni mara ya pili kwa muswada huo kukwama kuwasilishwa bungeni kutokana na sababu mbalimbali, ambapo awali Serikali ilipanga kuupeleka bungeni Novemba mwaka jana, lakini ilishindikana kwa maelezo kwamba, wadau wapate nafasi ya kutosha kutoa mapendekezo yao juu ya marekebisho hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!