Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko TEF yaendelea kumng’ang’ania Nape epeleke muswada wa habari bungeni
Habari Mchanganyiko

TEF yaendelea kumng’ang’ania Nape epeleke muswada wa habari bungeni

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limesema linatarajia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, atatimiza ahadi yake ya kupeleka bungeni jijini Dodoma, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Balile ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, tarehe 19 Januari 2023, akizungumza katika ofisi za TEF zilizoko Kisutu, jijini Dar es Salaam.

“Mwezi huu tunatarajia kwamba Wizara ya Habari itawasilisha muswada wa huduma za habari bungeni kama waziri (Nape Nnauye) alivyoahidi mara kadhaa kwamba utaingia bungeni, utajadiliwa na Mungu akipenda Februari 2023 utapitishwa na kuwa sheria tuanze utaratibu mwingine wa kuunda vyombo vinavyotakiwa ikiwemo Baraza Huru la Habari na kuangalia utunzi wa kanuni zitakazotokana na mabadiliko mbalimbali,” amesema Balile.

Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)

Balile amesema kuwa, maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kuhusu maboresho ya sheria za habari, yanaanza kufanyiwa kazi na hivyo muelekeo wake ni mzuri.

“Sasa tuna hamu kubwa kuona kwamba muswada huo unaingia baada ya kushindikana katika Bunge la Februari , Septemba na Novemba 2022. Lakini tulikwisha zungumza na waziri na watendaji serikalini hivyo ni matumaini yetu makubwa sana tunataraji tutauona muswada huo ukiingia bungeni na mambo yote yaweze kwenda vyema,” amesema Balile.

Serikali ya Tanzania ilichelewa kuwasilishwa Muswada huo bungeni, ili kuwapa nafasi ya kutosha wadau kutoa maoni yatakayosaidia upatikanaji wa sheria bora na rafiki kwa sekta ya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!