Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Tangulizi TEF wakomalia mabadiliko sheria ya habari
Tangulizi

TEF wakomalia mabadiliko sheria ya habari

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amesema kusudio la maboresho ya sheria za habari nchini, yanalenga kuwaondoa wanahabari na vyombo vyao katika vitanzi mbalimbali. Anaripoti Faki Sosi, dar es Salaam … (endelea).

Amesema moja ya kitanzi katika tasnia ya habari, ni kosa la mwandishi kufanywa kuwa kosa la kituo ama taasisi ya habari.

Amesema kosa la mwanahabari limekuwa likichukuliwa kama kosa la taasisi ya habari na kusababisha madhara makubwa ya kufungwa kituo ama gazeti tofauti na ilivyo kwenye tasnia nyingine nchini.

Akizungumza kwenye Kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Televisheni leo tarehe 28 Julai, 2022, jijini Dar es Salaam, mwenyekiti huyo amesema suala hilo ni miongoni mwa mabadiliko yanayopigiwa chapuo.

“Kosa la mwandishi mmoja, unafungia kituo ama gazeti? Kuna watu wengi wanaumia hapo. Yupo dereva ambaye wala hahusiki na habari iliyochapishwa lakini hata mwananchi ambaye hupata Habari kwenye chombo anachokipenda, anakuwa ameumizwa” amesem Balile.

Ametoa mfano wa daktari aliyemfumua nyuzi mgonjwa baada ya kushindwa kulipa Sh. 10,000 gharama za matibabu “huyu daktari, waziri hakumfukuza kazi, alimpeleka kwenye bodi ya madaktari na wao wakachukua hatua stahili.”

Amesema iwapo Bodi ya Ithibati ya Habari itakuwa huru na kujumuisha wadau mbalimbali wa tasnia hiyo, itakuwa na ufanisi mkubwa na kujengea heshima tasnia hiyo.

Pia amesema, mchakato wa mabadiliko ya sheria kandamizi za habari nchini, haulengi upendeleo kwa wanahabari bali haki, wajibu na mazingira mazuri ya tasnia hiyo.

“Mchakato wa mabadiliko haya, unalenga kuweka mipaka lakini pia uhuru wa habari bila kuumiza mtu yeyote. Tunalenga kupata uhuru zaidi wa habari na wajibu kwa mwanahabari.

“Tunapozungumzia uhuru wa vyombo vya habari, sio kwamba tunataka upendeleo kutoka serikalini, la! Tunacholenga hapo kila mmoja apate haki na awajibike,” amesema Balile.

Aidha, Balile amesema ingawa wadau wa habari wanasimamia mabadiliko hayo, uhuru wa habari unawahusu hata wale wasio wanahabari.

Kwamba, nchi ambayo uhuru wa habari haupo, wananchi hukosa fursa ya kupata taarifa sahihi na hivyo kunyima haki yao ya msingi ya kuhabarika.

“Tufahamu kuwa uhuru wa habari ni haki ya msingi ambayo wengine wanaitaka. Vyombo vya habari visipokuwa huru, wananchi nao pia wanakosa uhuru ikiwa ni pamoja na kutoa maoni yao pia kupata taarifa zinazowahusu moja kwa moja,” amesema.

Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kupitia sheria za habari na kuagiza zifanyiwe maboresho ili kuendana na mazingira yaliyopo.

“Tulikutana na rais (Rais Samia) Ikulu na kwa kuanza, tulimuomba kuhamisha tasnia ya habari na kuipeleka kwenye Wizara ya Mawasiliano, tunashukuru amefanya hivyo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!