JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumfungulia Mwanahabari wa gazeti la Tanzania Daima, Sitta Tuma mashitaka ya kuandamana bila kibali. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Tamko la TEF lilitolewa hapo jana Agosti 9, 2018 na Kaimu Mwenyekiti wake, Deodatus Balile ambapo alisema mwanahabari huyo alikuwa kazini akitekeleza wajibu wake wa kukusanya habari.
Tuma alikamatwa Agosti 8 mwaka huu pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na wafuasi 18 wa chama cha Chadema wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya mgombea udiwani wa chama hicho Kata ya Turwa.
Wakati TEF likipinga kukamatwa kwa mwanahabari Tuma, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana lilitoa tamko la kulaani tukio la shambulio lililodaiwa kufanywa na polisi kwa mwandishi wa habari za Michezo, Sillas Mbise lililotokea katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Asante Kotoko kutoka Ghana uliofanyika uwanja wa Taifa juzi Agosti 8, 2018.
Kufuatia kadhia hiyo, TFF imesema imekutana na viongozi wa Chama cha waandishi wa habari za michezo nchini TASWA na kujadiliana kuhusu tukio hilo na hatua stahiki zitachukuliwa.
Leave a comment