September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TEF: Mwakyembe amekurupuka

Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Spread the love

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa tamko la kulaani kitendo cha Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kulifungia gazeti la MAWIO na kusema vifungu vya sheria vilivyotumika si sahihi, anaandika Mwandishi Wetu.

Theophil Makunga, mwenyekiti wa TEF amesema hatua iliyochukuliwa na Serikali kupitia Dk. Mwakyembe haikuzingatia umakini na weledi na badala yake hisia zilitangulizwa zaidi.

“Kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 alichotangaza waziri kuwa amekitumia kulifungia gazeti la MAWIO, hakimpi mamlaka ya kufunga chombo cha habari bala kinampa mamlaka ya kuzuia taarifa au chapisho ikiwa linahatarisha amani ya nchi,” amesema Makunga.

Amesema jukwaa la wahariri limeshtushwa na kitendo cha waziri kujivika mamlaka ya kulifungia gazeti badala ya kulishtaki mahakamani kama sheria hiyo inayoeleza.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian Jesse Kwayu amesema waziri Mwakyembe anapaswa kujipima kama bado ana uhalali wa kuendelea kuishikilia nafasi aliyonayo kwani amejikita kwenye kupambana na vyuombo vya habari badala kuvilea.

“Kwa tukio hili la kuifungia MAWIO ni vyema Waziri Mwakyembe ajitafakari kama kweli anafaa kuendelea kwenye nafasi hiyo. Atambue kuwa yeye si bwana jela aliyeenda kwenye wizara ile bali ni waziri wa habari anayepaswa kusimamia sheria na si kuzivunja,” amesema Jesse Kwayu, Mjumbe wa TEF.

error: Content is protected !!