August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TEF nao wamkaba koo Prof. Lipumba, wamtaka aombe radhi

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Theophil Makunga

Spread the love

JUKWAA la Wahariri Tanzania ‘TEF’ limemtaka Prof. Ibrahim Lipumba kutoa kauli kuhusu tukio la kupigwa kwa waandishi wa habari katika uvamizi wa mkutano wa Chama cha Wananchi ‘CUF’ uliotokea wiki iliypita, anaandika Hamisi Mguta.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Theophil Makunga katika mkutano wake na waandishi wa habari wakitoa msimamo wao kufuatia tukio hilo.

“Ufuatiliaji uliofanyika na TEF ikiwa ni pamoja na kuzungumza na uongozi wa pande mbili zinazovutana kwenye chama hiko umebaini kuwapo kwa viashiria kwamba mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yalifanywa na wanaomuunga mkono Prof. Lipumba,

“Tunamtaka Prof. Ibrahim Lipumba binafsi atoe kauli kuhusu tukio hilo kama alivyofanya Maalim Seif ambaye aliandika barua rasmi kwa uongozi wa TEF akilaani kupigwa kwa waandishi wa habari na kutoa pole kwa walioumizwa na kupata misukosuko,”amesema Makunga.

Amesema tukio hilo linaingilia uhuru wa vyombo vya habari kinyume cha sheria huduma ya habari ya mwaka 2016 na wanaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa mikutano ya kihabari ya Prof. Lipumba na wafuasi wake.

“Tunatoa wito kwa jeshi la Polisi kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika wa uhalifu huu, nasema tukirejea kukamatwa kwa mmoja wa watuhumiwa wa tukio hilo katika eneo la tukio,” amesema.

Miongoni mwa waandhishi wa habari walioathiriwa ni Fredy Mwanjala (Chanel ten), Asha Bani (Mtanzania), Mary Geoffrey (Nipashe), Mariam Mziwanda (Uhuru), Kalunde Jamal (Mwananchi), Rachel Chizoza (Clouds) na Henry Mwang’onde (The Guardian).

Siku moja kabla ya msimamo huo wa TEF, Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari wa CUF upande wa Prof. Lipumba alilikiri kuwa watu walioshambuliwa na wananchi kwa kigezo cha kuwa ni wavamizi walikuwa ni walinzi wa upande huo.

error: Content is protected !!