August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCU yajivua rasmi udahili wa wanafunzi

Eleuther Mwageni , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Spread the love

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imejivua rasmi jukumu la kusimamia suala la udahili kwa wanafunzi ambao wanatarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu mwaka huu , anaandika Hellen Sisya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya tume hiyo mapema leo hii, Eleuther Mwageni , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo amesema kuwa, wanafunzi wote watakaohitaji kujiunga na masomo ya elimu ya juu wanapaswa kutuma maombi yao kwa vyuo husika na siyo  TCU kama ambavyo imezoeleka miaka ya nyuma.

Aidha, tume hiyo imewaomba waombaji wote kusoma miongozo ya udahili ambayo inapatikana katika mtandao wa tume hiyo na kusisitiza kuwa waombaji wanapaswa kuomba kozi ambazo zinatambuliwa na TCU pamoja na NACTE ambazo pia zinapatikana katika mtandao wa tume hiyo.

Tume hiyo pia imetoa wito kwa vyuo vikuu kote nchini kutangaza kozi zinazotambulika na tume hiyo pamoja na kudahili wanafunzi wenye vigezo na sifa stahiki katika kila kozi.

Hapo awali, tume hiyo ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kudahili wanafunzi wanaojiunga na elimu juu nchini ambapo wanafunzi walikuwa wanatuma maombi yao kwa tume hiyo na tume hiyo inachukua jukumu la kuwapangia vyuo vya kwenda kusoma.
MWISHO

error: Content is protected !!