December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TCU yafuta chuo cha TIU

Spread the love

IKIWA ni siku 10 kupita baada ya mtandao huu kuripoti mgomo wa walimu katika Chuo cha Kimataifa cha Tanzania (TIU) kilichopo Kimara Stop-Over, Dar es Salaam, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekifutia leseni chuo hicho, anaandika Faki Sosi.

Walimu hao waligoma kuingia darasani kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao pamoja na kutopewa mikataba ya kazi.

Taarifa iliyotolewa na Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, chuo hicho kimefutiwa leseni yake kutokana na kushindwa kutimiza masharti yaliyobainishwa kwenye leseni iliyowepewa.

Mgaya ameleza kuwa, chuo hicho kimeanzisha kufundisha programu za astashahada na stashahada bila ithibati ya mamlaka husika na kuongeza TCU haitambui program zinazotolewa na chuo hicho.

error: Content is protected !!