August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCU yafafanua ada ya usajili wanavyuo

Eleuther Mwageni , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Spread the love

SERIKALI kupitia Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imeviagiza vyuo vikuu kote nchini kutoza kiasi cha pesa kisichozidi Sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi atakayeomba nafasi ya kujiunga na elimu ya juu katika vyuo hivyo, anaandika Hellen Sisya.

Edward Mkako, Afisa Habari wa TCU, amethibitisha kuwepo kwa agizo hilo.

“Ni kweli. Agizo hilo limetolewa na serikali leo hii katika maonesho ya vyuo vikuu ambayo yamefunguliwa leo hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja,” amesema Mkako na kuongeza:

“Kwa wanafunzi ambayo tayari wameshatozwa zaidi ya kiasi tulichotangaza, tunawaachia serikali, sisi hatuhusiki.”

Agizo hilo la serikali limekuja wakati huu ambao tayari baadhi ya wanafunzi wameshawasilisha maombi yao kwa vyuo kadhaa nchini na kukatwa kiasi cha pesa ambacho kinazidi kiasi ambacho kimetangazwa leo hii na serikali.

error: Content is protected !!