October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCU watia kitanzi vyuo viwili

TCU

Spread the love

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imevifuta vyuo vikuu viwili kikiwemo cha Mtakatifu Yohana (SJUT) kilichopo Msalato Dodoma na Theophil Kisanji (TEKU) cha Tabora na kusitisha utoaji mafunzo katika vyuo vikuu vitano. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 25 Septemba 2018 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amevitaka vyuo vilivyositishwa kutoa mafunzo kuwahamisha wanafunzi katika vyuo vilivyositishwa kuhamishwa katika vyuo vingine kabla ya muhula wa mwaka wa masomo wa 2018/19 kuanza.

Profesa Kihampa, amevitaja vyuo vilivyositishwa kutoa mafunzo ikiwemo Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo Kikuu cha Eckernford Tanga (ETU), Chuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta kituo cha Arusha (JKUAT-Arusha Center) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo).

Amesema vyuo hivyo viko katika uangalizi maalum na kwamba haviruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo kuanzia Astashahada, Stashahada, Shahada, Shahada ya uzamili na uzamivu.

error: Content is protected !!