June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCRA yawataka waandaa maudhui kuzuia yasiyofaa

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imewataka watoa huduma za mawasiliano nchini humo, kuzingatia sheria na kanuni zilizomo kwenye leseni katika utoaji wa huduma husika kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, imewataka kuhakikisha wanasimamia vyema mauadhui yasiyofaa yasiende kwa jamii.

Wito huo umetolewa jana Jumatano, tarehe 28 Julai 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabiri Bakari wakati wa kikao cha watoa huduma za utangazaji na maudhui kilichofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya wadau hao, ni Azam Media, Multchoice Tanzania limited, watoa huduma kwa njia ya Cable, Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na TFF. Pia, kikao hicho kilihudhuliwa na watoa huduma za utangazaji na maudhui kutoka vyombo vya habari mbalimbali.

Dk. Bakati alisema baadhi kanuni za maudhui na utangazaji zinafanyiwa maboresho na zinatarajia kuanza hivi karibuni

Alisema TCRA imeboresha utendaji kazi zake kwa kuweka mifumo madhubuti zaidi na imeendelea kutoa ushauri kwa watoa huduma kila mara.

Kikao hicho ambacho kimeratibiwa na TCRA, kanda ya kati, kililenga kutoa elimu ya namna bora zaidi katika kufikisha maudhui kwa walaji bila kuwa na migongano baina ya watoa huduma.

Pia kikao kimependekeza wanaochakata maudhui kuangalia namna nzuri zaidi ya kuzuia maudhui yasiyo na staha kwa jamii ili kuondoa malalamiko ndani ya jamii.

Mwisho wa kikao hicho cha siku moja, kimependekeza pia vikao kama hivyo kiwe kinafanywa mara kwa mara ili kuongeza ufahamu zaidi kwa watoa huduma na mamlaka za serikali zinazosimamia sekta ya maudhui ya utangazaji.

error: Content is protected !!