Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRA yafungia laini 52,000
Habari Mchanganyiko

TCRA yafungia laini 52,000

Spread the love

 

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefungia namba za simu 52,087, zilizojihusisha na wizi, utapeli na ulaghai kupitia mtandao wa simu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 8 Novemba, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari, ambapo alifafanua namba hizo zimeripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu hivyo zimezuiliwa kupokea na kutoa huduma za mawasiliano.

“Kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Septemba 2022 jumla ya namba tambulishi (IMEI) zilizofungiwa na mfumo huu ni 52,087 ambazo ziliripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu, hivyo kuwezesha kupunguza matukio ya wizi na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mawasiliano vyenye ubora kwenye soko,” alisisitiza Bakari.

Alieleza kuwa, kupitia kanzidata ya Namba Tambulishi, moduli hiyo imewezesha uhakiki wa vifaa vyote vinavyounganishwa na mitandao ya watoa huduma kama vinakidhi viwango vya kimataifa na ni salama kwa watumiaji.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari

“Moduli hiyo iliyopo katika Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) imewezesha kuzuia matumizi ya simu zilizoripotiwa kuibiwa, kupotea au kuharibika pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.

Usimamizi huu unawezesha kubaini na kufungia namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano zilizonakiliwa (Duplicate IMEIs), namba tambulishi za vifaa vilivyotumika kwenye udanganyifu pamoja na namba tambulishi zilizotolewa taarifa ya kupotea au kuibiwa,” aliongeza.

Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya wananchi akiwemo Mpoki Mwakabinga mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam aliishukuru TCRA kwa jitihada inayofanywa kuhakikisha uhalifu mtandaoni hasa unaohusisha vifaaa vya mawasiliano kiganjani unatokomezwa kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Tunaishukuru TCRA, hakika inajitahidi sana kuwalinda wananchi kupitia mifumo yake ya usimamizi wa mawasiliano, hawa matapeli wamekuwa wengi kiasi kwamba tunakuwa na wasiwasi, kama wanafungiwa hili ni jambo la heri,” alibainisha Mpoki.

Mamlaka hiyo awali ilieleza kuwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu mara wanapobaini kupokea simu au ujumbe mfupi wa maandishi wenye viashiria vya utapeli wanapaswa kutoa taarifa kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno “utapeli” kwenda namba 15040 na kutuma namba ya tapeli kwenda namba hiyohiyo.

Aidha TCRA ilisisitiza kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano ahakikishe anahakiki namba zake za simu zilizosajiliwa kwa njia ya kibayometria, kwa kutumia namba ya kitambulisho cha Taifa wanapaswa kubofya *106# kisha kufuata maelekezo. Hatua ambazo Mamlaka hiyo ilieleza zinasaidia kupunguza utapeli kwa njia ya simu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!