Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko TCRA wawaburuza wamiliki wa YouTube kinyemela
Habari Mchanganyiko

TCRA wawaburuza wamiliki wa YouTube kinyemela

Spread the love

WATU wanne wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la kuchapisha maudhui ya YouTube bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Anaripoti Danson Kaijage … (endelea)

Washitakiwa hao ambao wamefikishwa mbele ya mahakama hiyo, wametajwa majina yao kuwa ni Charles Kombe (24) mkazi wa Mikocheni, John Chuwa (28), mkazi wa Barakuda, Amos Warema (27) na Raymond Mkoroka (30). 

Wote kwa pamoja wanadaiwa kuchapisha mtandaoni maudhui hayo katikà tarehe tofauti kati ya mwaka 2018 na Mei mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Wakili wa serikali, Elizabert Mkunde ameieleza Mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando kuwa, kati ya Agosti 1 ,2017 na Mei 21, 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam watuhumiwa hao walibainishwa kujihusisha na vitendo hivyo vya kiharifu kwa kutumia mtandao wa YouTube bila kuwa na kibali.

Wakili Mkude amesema kuwa mshtakiwa Kombe alichapisha maudhui mbalimbali hayo kupitia mtandao wake wa Youtube uitwao Charles Kombe bila kibali.

Hata hivyo, mshtakiwa Kombe amekana kutenda kosa hilo kutokana na mshitakiwa kukana mashitaka  yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh. 5 milioni kila mmoja.

Mshitakiwa Chuwa, amesomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde ambapo imedaiwa, kati ya mwaka 2018 na Aprili 2019 jijini Dar es Salaam mshtakiwa alichapisha maudhui kupitia mtandao wa Youtube uitwao John Film Entertainment bila ya kuwa na kibali kutoka TCRA.

Mshtakiwa Chuwa amekiri kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kujidhamini mwenyewe kwa bondi ya Sh. 5 milioni.

Baada ya mshitakiwa kukubali kosa Kesi yake imeahirishwa hadi Juni 7 mwaka huu, mbapo mshitakiwa atakaposomewa maelezo ya awali.

Katika kesi nyingine iliyosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega, wakili wa serikali Candid Nasua ameieleza mahakama kuwa kati ya Novemba 2018 hadi Mei 17 mwaka huu katika maeneo tofauti katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam mshitakiwa Warema, alisambaza maudhui hayo kupitia mtandao wa Youtube uitwao Pro Media Tanzania bila kuwa na kibali kutoka TCRA.

Mshitakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka  kujidhamini mwenyewe na kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh. 5 milioni.

Baada ya mshitakiwa kukubali kutenda kosa kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kwa upande wake, mshtakiwa Mkoroka naye alisomewa shitaka lake  na wakili wa serikali Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Rwezile.

Mshitakiwa amekana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kuwa na mdhamini mmoja na kujidhamini mwenyewe kwa kusaini bondi ya Sh. 5 milioni.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 4 mwaka huu itakapotajwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!