February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TBS yapiga ‘stop’ tairi zilizotumika

Spread the love

SHIRIKA la Viwango Nchini (TBS) limepiga marufuku matumizi ya tairi za vyombo vya moto zilizotumika na kuisha muda wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 24 Oktoba 2018 na TBS kupitia Mkurugenzi Mkuu wake, Dk. Ngenya Yusuf.

“TBS inapenda kuwakumbusha waagizaji na watumiaji wa tairi za magari kuwa umri wa tairi za magari ni miaka nane kutoka tarehe ya kutengenezwa kwake ambayo imeanishwa katika kila tairi. Tairi halitafaa kutumika baada ya umri huo bila kujali kuwa halijawahi kutumika kabisa,” inaeleza sehemu ya taarifa ya TBS.

Sambamba na marufu hiyo, TBS imepiga marufuku wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa tairi za magari, pikipiki na baiskeli, kuuza na kutumia tairi hizo zilizotumika.

Vile vile, TBS imetangaza kufanya msako katika maduka ya tairi ili kubaini wauzaji watakao kiuka agizo hilo kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria.

Tangazo hili litaenda sambamba na ukaguzi utakaofanyika kwenye soko kwa lengo la kubaini watakao kiuka agizo hili kwa kuendelea kufanya biashara ya kuuza au kusambaza tairi ambazo zilishatumia.

error: Content is protected !!