January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TBS yakifungia kiwanda cha maziwa Kilimanjaro

Kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Creamers kilichofungiwa

Spread the love

SHIRIKA la Viwango TBS limekifunga Kiwanda cha Maziwa na siagi cha Kilimanjaro Creamers kinachofanya shughuli zake Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro baada ya kubainika kuzalisha bidhaa zisizothibitishwa viwango na kutumia vibaya nembo ya shirika hilo kinyume cha sheria. Anaandika Ferdinand Shayo, Kilimanjaro … (endelea).

Maafisa wa TBS walifika kiwandani hapo ambamo shughuli za uzalishaji zilikua zikiendelea huku mmiliki wa kiwanda hicho akiwa nje ya Ofisi ambapo waliingia na kufanya ukaguzi baada ya kujiridhisha na ushahidi waliamua kukifunga kiwanda hicho.

Afisa Mahusiano wa TBS, Roida Andusamile amesema kuwa bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo hazijathibitishwa iwapo zinakidhi viwango vya ubora jambo ambalo linaweza kuathiri afya za watumiaji hivyo wameamua kukifunga kiwanda hicho .

“Baada ya kufanya uchunguzi na kujiridhisha tumeamua kufunga kiwanda hiki ambacho kinatumia nembo za TBS katika bidhaa wakati bado bidhaa hizi hazijathibitishwa na shirika la viwango hivyo tunakifunga mpaka pale watakapothibitisha ubora wa bidhaa zao” Amesema Roida.

Afisa Mdhibiti Ubora na Mkaguzi wa TBS Matrona Emmanuel amesema kuwa kiwanda hicho kimekua kikitumia namba feki za uthibitisho na nembo za kitendo ambacho ni udanganyifu mkubwa kwa umma na TBS haitaweza kuwafumbia macho wazalishaji na wamiliki wa Viwanda wanaokiuka taratibu za usajili.

“Hatujawahi kuthibitisha ubora wa bidhaa zetu mfano hii ya maziwa (cultured milk) TZS 1220 kiwango ambacho si sahihi ilitakiwa iwe TZS 251 kulingana na kiwango cha maziwa fresh ,tumeamua kufunga kiwanda hiki kwa sababu anawadanganya wateja “ Amesema Matrona

Afisa Sheria wa TBS ,Yunus Lema amesema kuwa kutokana na kosa hilo mkosaji atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 50 ama kifungo cha miaka 2 ama adhabu zote mbili kwa mujibu wa sheria.

Amesema mapambano dhidi ya bidhaa zisizothibitishwa viwango vya ubora na TBS yanaendelea ,jamii na wadau mbali mbali wanalo jukumu la kushiriki katika vita hiyo ili kulinda afya za watanzania walio wengi ambao ndio waathirika wakubwa wa bidhaa hizo.

error: Content is protected !!