August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TBS kutumia Sh 9.9 bilioni kujenga maabara Dodoma, Mwanza

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dk. Athuman Ngenya

Spread the love

 

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetenga kiasi cha Sh. 9.9 Billioni kwa ajili ya kujenga jengo la maabara (Viwango House) katika miji ya kimkakati ya Dodoma na Mwanza ili kusogeza huduma za Shirika karibu kwa wateja na kuongeza ufanisi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu tarehe Mosi Agosti, 2022 na Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Dk. Athuman Ngenya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya vipaumbele na mikakati yao katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akielezea vipaumbele hivyo amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023, Shirika limeandaa vipaumbele kwa kuzingatia Mpango mkakati wa Shirika wa mwaka 2021/2022- 2025/2026.

Aidha ameeleza kuwa Shirika limetenga kiasi cha Sh. 2.7 Billioni kwa ajili ya kuimarisha ofisi saba za kanda ambazo ni Arusha, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma na Mbeya, kwa kuongeza wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama.

Amezidi kueleza kuwa Shirika limetenga Sh. 1.6 Billioni kwa ajili ya kuandaa viwango 630 vya kitaifa katika sekta mbalimbali ili kuwezesha biashara kwa kumpa mzalisaji uhakika wa kupata masoko ya ndani na nje na kumhakikishia mlaji wa mwisho usalama na ubora wa bidhaa atakayotumia ikiwa ni pamoja na kuweka ushindani sawia wa bidhaa katika soko.

Ameongeza kuwa Shirika limetenga Sh. 261 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi ili kuhakikisha wananchi wanatumia bidhaa zilizo bora na salama.

Ameeleza zaidi kuwa Shirika limetenga Sh. 581 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uthibitishaji wa mifumo ya kiutendaji ambapo kwa sasa TBS imepatiwa ithibati ya kufanya shughuli hiyo na mashirika yanayoweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia TBS.

Amesema kuwa mifumo hiyo itasaidia kuhakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Katika vipaumbele vingine amesema Shirika limetenga Sh. 800 Millioni kwa ajili ya kufanya shughuli za kuhakiki ubora wa vipimo “ili kuhakikisha usahihi wa majibu ya vipimo mbalimbali kutokea maabara, mahospitalini na viwandani na kupelekea watoa huduma kufanya maamuzi sahihi.”

Pia amesema Shirika limetenga Sh. 1.18 Billioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini (PVoC) na baada ya kuwasili nchini (Destination Inspection) ili kuhakikisha nchi haiwi jalala la kupokea bidhaa zilizopigwa marufuku au hafifu.

error: Content is protected !!