July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TBL yawatunuku wafanyakazi wake

Spread the love

KAMPUNI  ya  bia  ya TBL Group imewatunuku vyeti na zawadi wafanyakazi wake ambao wameitumikia kwa muda mrefu. Anaandika Aisha  Amran …(endelea)

 Wafanyakazi walionufaika na  na zawadi hizo ni wanaofanya kazi katika viwanda vya Konyagi, Chibuku na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika  jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Mkurugenzi wa Ufundi, Gavin Van Wijk,  amewapongeza wafanyakazi kwa uvumilivu na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utumishi wao.

Wijk amesema kampuni hiyo itaendelea kuwajali wafanyakazi wake na kuwajengea mazingira bora ya kazi kwa lengo la kutoa mchango mkubwa zaidi kwa taifa, kwa taasisi na taifa kwa ujumla.

“Tunaamini kuwa wafanyakazi wetu wote ni  familia moja hivyo siku zote tutakuwa nao karibu na kuendelea kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi. Naamini sote tukishirikiana tutafanikiwa na kuendelea kupata mafanikio,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa TBL kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin, amesema wafanyakazi hao ni mfano wa kuigwa na kuwataka wengine, hususani vijana, kufanya kazi kwa bidii na kuwa wavumilivu.

“Tuko hapa kwa ajili ya kuwapongeza wenzetu ambao wamefikia siku hii kupewa tuzo ya utumishi wa muda mrefu. Ninaamini sote tukifanya kazi kwa bidii na kuwa na uvumilivu, tutafanikiwa kufikia hatua kama waliyofikia wenzetu ambao tunawapongeza,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake waliotunukiwa vyeti, Sylvester Kunambi ambaye ametumikia kampuni kwa  miaka 35, amesema siri kubwa ya utumishi wa muda kwenye kampuni ya TBL ni kutokana na mazingira bora ya kazi .

Wafanyakazi 25 waliotumikia kampuni katika kipindi cha miaka 10 mpaka miaka 35 walitunukiwa vyeti.

error: Content is protected !!