Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Tatizo la uhaba wa sukari mwisho 2025/26
Habari Mchanganyiko

Tatizo la uhaba wa sukari mwisho 2025/26

Sukari
Spread the love

SERIKALI imeeleza kuwa ifikapo mwaka 2025/26 Tanzania itakuwa na sukari ya kutosheleza  matumizi ya ndani  na akiba ya kuuza nchi za nje kwa kuzalisha tani zaidi ya 756,000 kwa mwaka. Anaripoti Danson Kaijage,Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 25 Oktoba 2022 na Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Kenneth Bengesi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya bodi hiyo katika mwaka wa fedha 2022/23 katika ukumbi wa mikutano wa Habari Maelezo jijini Dodoma.

Prof. Bengesi amesema kuwa kutokana na juhudi ambazo zinafanywa na serikali ili kuhakikisha sukari inapatikana nchini kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya ndani na ziada ya kuuza nje.

Sambamba na hilo Prof.Bengesi ameeleza kuwa licha ya kuwepo na uhaba mkubwa wa sukari kwa kuwa na sukari isiyo tosheleza lakini kwa sasa Serikali imewezesha kwa kiasi kikubwa katika sekta ya sukari ili kupata sukari ambayo itatosheleza mahitaji.

“Toka kuanzishwa kwa bodi ya Sukari Tanzania haijawahi kujitoshereza katika sekta ya sukari tumekuwa tukitumia fedha nyingi kuagiza sukari nje ya nchi. Na ninaposema matumizi ya sukari naongelea maeneo makubwa mawili ya matumizi ya sukari kwani kuna sukari ya matumizi ya sukari ya majumbani na matumizi ya viwandani.

“Lakini tumekuwa na upungufu mkubwa wa sukari na itambuliwe kuwa Tanzania haijawahi kuzalisha sukari ya viwandani hivyo inalazimika kuagiza sukari ya viwandani kutoka nje ya nchi.

Amesema wamekuwa wakitumia takribani dola za kimarekani milioni 150 sawa na fedha za kitanzania Sh. 300 bilioni kwa mwaka.

Pamoja na mambo mengine amesema Bodi ya sukari tayari imefanya utafiti kwa ajili ya kubaini maeneo ambayo yanaweza kulima zao la miwa na kuona uwezekano wa kusimika viwandani vidogo vidogo kwa lengo la kupunguza uhaba wa sukari.

Kuhusu sukari ya viwandani Prof. Bengesi amesema kuwa serikali inafanya juhudi ya kuwekeza kwa ajili ya kuzalisha sukari ya viwandani na kuepukana na suala la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa iwapo Tanzania itaanza kuzalisha sukari ni wazi watakuwa wameongeza ajira kwa vijana na upatikanaji wa fedha za kigeni pale ambapo watakuwa wapo tayari kuuza bidhaa hiyo nje.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!