Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Tatizo la mdomo wazi linatibiwa bure CCBRT’
Habari Mchanganyiko

‘Tatizo la mdomo wazi linatibiwa bure CCBRT’

Spread the love

WAZAZI wenye watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo wazi (Mdomo Sungura), wametakiwa kuwapeleka hospitali kwa ajili ya upasuaji. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Akizungumza leo tarehe 4 Oktoba 2019, na Waandishi wa Habari katika Hospitali ya CCBRT, Msasani jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya tabasamu, Daktari wa Masuala ya Mifupa Dk. Zainab Ilonga amesema, tatizo hilo linatibika.

Amesema, watu wengi wanahusisha hali hiyo na imani ambazo sio sahihi na uhalisia wa chanzo cha tatizo hilo, na kwamba tatizo hilo hutokea kutokana na matatizo wakati mimba ikiendelea kukua au kwa kurithi.

“Hili ni tatizo ambalo mtoto anazaliwa nalo, na huwa linatokea wakati ujauzito bado unaendelea kukua tumboni. Kipindi cha nwanzo wa ujauzito, mdomo wa nje na mdomo wa ndani vya mtoto huwa vinajifunga kukutana kwa pamoja, inaweza ikatokea kitendo hicho kikashindikana na ikapekekea mtoto kuwa na tatizo hili,” amesema.

Amesema, takwimu za dunia zinaonesha kuwa, kati ya watoto 700 wanaozaliwa, mtoto mmoja anazaliwa na tatizo la mdomo wazi ambapo wataalam bado hawajagundua chanzo chake ingawa wananasibisha na matumizi ya sigara wakati wa ujauzito, kuwa mnene sana au kuwa na kisukari wakati wa ujauzito.

“Hivi ni vitu ambavyo vinaweza kupelekea mama mjamzito kuopata mtoto wa namna hii, lakini inawezekana alikuwa havuti sigara,” amesema.

Jane Ngige, Mkurugenzi wa Shirika la Smile Train Afrika Mashariki linalosaidia watoto hao kufanyiwa upasuaji bure amesema, tasamu ni kitu muhimu hivyo uso ndio una muonekano wa mtu akitabasamu na ndio maana kutibu watoto hao.

“Tanzania zaidi ya watoto 2,500 wanazaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo hili na shida ni nyingi. Wengi wao hawajui kwamba usaidizi upo hivyo, Smile Train tumeamua kusaidiana na CCBRT kutoa matibabu bure,” amesema.

Amesema, wanashirikiana na hospitali takribani nane kutoka Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Shinyanga na Mbeya, na watoto wote wanaokwenda kwa ajili ya kupata matibabu hayo, ni bure.

“Tunafurahi kuwa hapa na sasa tumesaidia zaidi ya watoto 2,000 na tutaendelea na hii huduma, tunaomba watoto wenye matatizo hayo wajitokeze ili watibiwe,” amesema.

Veronica Cristopher, Mkazi wa Goba ambaye mtoto wake amezaliwa na tatizo hilo amesema, mwanaye hakuwahi kutengwa ila baadhi ya watu wananyanyapaa watoto wa aina hiyo.

“Baada ya kujifungua huyu mtoto, alikuwa na tatizo la mdomo lakini nilielekezwa kuja hapa na nikafanya hivyo sasa na subiri ili afanyiwe upasuaji,” amesema.

Neema Ally, ambaye mtoto wake amefanyiwa matibabu amesema, hakuwahi kutengwa kwa hivyo, hakuwa na changamoto na sasa anafurahi kumuona mwanaye amepata matibabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia apandisha kikokotoo kutoka asilimia 33-40

Spread the loveHATIMAYE Serikali imesikia kilio cha wastaafu wa utumishi wa umma...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Polisi wamtia mbaroni RC wa zamani aliyedaiwa kulawiti

Spread the loveJeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wafungwa, mahabusu ruksa kupiga kura

Spread the loveTUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa wafungwa,...

error: Content is protected !!