Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tatizo la Luku: Majaliwa atoa maagizo mengine ‘wakae pembeni’
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tatizo la Luku: Majaliwa atoa maagizo mengine ‘wakae pembeni’

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dk. Merard Kalemani
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amemuagiza Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, asiishie kuwasimamisha kwa siku kumi tu meneja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na wasaidizi wake, bali wakae pembeni hadi hapo uchunguzi zaidi utakapokamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Jana Jumatano, Dk. Kalemani, aliwasimamisha kazi kwa siku kumi, Meneja wa Tehama na Huduma za Biashara wa Tanesco, Lonus Feruzi na wasaidizi wake wawili, Frank Mushi na Idda Njau.

Aliwataka watoe maelezo kufuatia kuwepo kwa tatizo katika huduma ya manunuzi ya LUKU kupitia njia za kielektroniki, lililodumu kwa siku tatu kuanzia Jumatatu hadi jana usiku huduma hiyo iliporejea.

Kutokana na tatizo hilo, huduma hiyo ya luku ilikuwa ikipatikana ofisi za Tanesco, mkoa na wilaya hivyo kusababisha adha kwa wananchi.

Kutokana na kadhia hiyo, Majaliwa leo asubuhi Alhamisi, tarehe 20 Mei 2021, amekutana na Menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), makao makuu ya zamani Shirika hilo, Ubungo, mkoani Dar es Salaam.

“Lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote. Hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo. Inawezekana sio wao tu, Waziri endelea na uchunguzi.”

Aidha, Majaliwa ameliagiza, shirika hilo kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa dharura ‘backup’ utakaotumika pindi kunapotokea changamoto za kimfumo

“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu”

Amesema, Serikali inataka kuona huduma hii inapatikana muda wote. “Jitihada za Serikali kuimarisha vyanzo vya umeme zina lengo la kuhakikisha tunapata umeme mwingi na wa gharama nafuu”.

Naye, Waziri wa Nishati Dk. Kalemani amesema, hakuridhishwa na watendaji wanaosimamia mfumo na amewaomba radhi Watanzania kwa usumbufu uliojitokeza.

Pia, amesema amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati aunde kikosi kazi maalum kwa ajili kuupitia upya mfumo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

error: Content is protected !!