July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Tatizo la ajira ni sera’

Spread the love

TATIZO la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini linasababishwa na sera ambazo serikali imezianzisha na kusimamia utekelezaji wake katika sekta ya elimu. Anaandika Eunice Laurian.

Hayo yameleezwa leo jijini Dar es Salaam kwenye mdahalo wa wazi kuhusu ajira kwa vijana ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Mdahalo huo ulioandaliwa na ubalozi wa Uswisi nchini umefanyika ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hiyo na Tanzania.

Washirika kwenye mjadala huo walijadili kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana na kuependekeza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaonekana kukua kwa jinsi siku zinavyokwenda.

Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza amesema kuwa ili serikali ipunguze tatizo la ajira kwa vijana inatakiwa kuhakikisha inaimarisha uchumi wa nchi ambao unatoa nafasi za ajira zaidi.

Amesema, mbali na kuimarisha uchumi pia inatakiwa kuwatengenezea wananchi wake mazingira mazuri ambayo yatawashawishi kujiajiri bila kutegemea serikali au kampuni binafsi ambayo kwa sasa ndiyo zinaonekana kutoa nafasi nyingi za ajira.

Aidha amewataka vijana kuacha tabia ya kutegemea ajira za serikali na sekta binafsi kwani ushindani katika soko la ajira ni mkubwa na kwamba, kama hawajajiandaa kwa kiasi kinachohitajika sasa katika soko la ajira, basi inaweza kuwa vingumu kwao kupata nafasi.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kuwa, zaidi ya vijana 800,000 humaliza chuo kila mwaka na wanaokadiriwa kupata ajira rasmi ni 40,000 pekee.

 

error: Content is protected !!