Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Taswo yampongeza Rais Samia kuigawanya wizara ya afya
Habari za Siasa

Taswo yampongeza Rais Samia kuigawanya wizara ya afya

Katibu Mtendaji wa Chama cha Wataalamu na Wanataaluma wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO), Furaha Dimitrios
Spread the love

 

CHAMA cha Wataalamu na Wanataaluma wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO), kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wa kutangaza kuigawanya wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

TASWO wametoa pongezi hizo ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Samia kutangaza uamuzi huo ili kutoa msukumo katika utekelezaji wa mipango na sera za masuala ya usawa wa kijinsia.

Rais Samia alisema ataigawa wizara hiyo itakayoshughulikia jinsia, wanawake na mambo mengine.

Katibu Mtendaji wa chama hicho, Furaha Dimitrios akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa, tarehe 17 Desemba 2021 amesema uamuzi huo wa Rais Samia itasaidia utekelezaji wa majukumu ya idara mbili ya Idara kuu ya Afya na ya Maendeleo ya Jamii.

Amesema kwani zimebeba majukumu makubwa ambayo utekelezaji, ufuatiliaji, usimamizi na uratibu wake umekuwa na changamoto katika kuwafikishia huduma bora za Ustawi wa jamii wananchi hasa makundi maalumu na watu wenye uhitaji maalumu.

Amesema Katika kufanikisha malengo mazuri ya Rais Samia ikiwemo kuwepo kwa “Kizazi chenye usawa” kama sehemu ya Tanzania kutekeleza lengo la maendeleo endelevu kidunia na kuboresha huduma za ustawi wa jamii na Maendeleo ya Jamii nchini, kuitenganisha Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii na Afya ni jambo muhimu na lenye tija.

“Kimsingi huduma za Ustawi wa Jamii zimekuwa ni huduma mtambuka toka Uhuru, na zimekuwa ni huduma muhimu katika kuzuia matatizo ya kijamii yanayoweza kuathiri jamii na hasa makundi maalumu lakini pia kuhudumia wale walioathirika na wenye mahitaji mbalimbali,” amesema Dimitrios.

Amesema makundi haya ni pamoja wanawake na wasichana ambao ni waathirika wakubwa wa mabadiliko ya kiuchumi, maendeleo, utamaduni na siasa kama Rais alivyosema, “watoto wote na hasa yatima, watoto wa mitaani na wanaokinzana na sheria.”

“…watoto walio katika mazingira hatarishi, watu wenye ulemavu, wazee, waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, wahanga wa matumizi ya madawa ya kulevya, wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, wahanga wa majanga mbalimbali ya kimazingira na kibinadamu, wagojwa wasioweza kumudu gharama za matibabu, wagonjwa wenye magonjwa ya muda mrefu yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa (wanaoishi na VVU, Shinikizo la damu, Kisukari, Shida ya figo, Kansa, magonjwa ya afya ya akili na kwa sasa janga lilililoikumba dunia la UVIKO19 na mengineyo),” amesema.

Dimotrios amesema makundi yote hayo yamekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia zikiwemo familia zenye migogoro na makundi mengine maalumu kutokana na athari mbalimbali.

“Kitengo hiki kimebeba wataalam wa huduma za ustawi wa jamii wanaotoa huduma kwa makundi tuliyoyataja hapo juu katika maeneo tofauti tofauti ndani na nje ya serikali,” amesema

Amesema wataalamu wa ustawi wa Jamii duniani kote wamepewa wajibu wa kushughulika na makundi maalumu kwa sababu utoaji wa huduma hizo unaongozwa na maadili, misingi na miiko ya taaluma yao kama ilivyo kwa kada za afya.

Amesisitiza kwa miaka mingi sekta ya ustawi wa jamii nchini haijapata nafasi inayostahili kimuundo na hivyo kuathiri huduma za ustawi wa jamii kwa makundi yote yaliyotajwa licha ya kuwa na sera, sheria na miongozo mbalimbali inayoongoza utoaji wa huduma hizo.

2 Comments

  • Safi Sana.
    Nayo Tanzania Revenue Authority (TRA) imekuwa inafuja mapato ya ushuru na forodha pale bandaging.
    Hivyo, ushuru na forodha iondolewe huko na kuwa Idara inayojitegemea. Hii itasaidia kuona mapato ya biashara na uingizaji hayawiani na kushughulikia ufujaji kwa haraka zaidi.
    Idara ya Income Tax na Revenue zibakie huko pamoja. Haya ni mapato ya uuzaji wa ndani.
    Ushuru na forodha ni mapato ya uuzaji wa nje, upitishaji wa mizigo, na uingizaji bidhaa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!