January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taswira ya Dodoma kuelekea Bunge la 11

Spread the love

WAKATI wabunge wateule wakitarajiwa kuwasili mjini Dodoma, mandalizi ya kuwapokea yanaendelea ambapo leo utaanza rasmi utaratibu wa usajili kwa wabunge hao. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na usajili wa wabunge hao kwa ajili ya Bunge la 11, maandalizi ya usafi katika viwanja vya bunge yanaendelea huku kampuni ya usafi ya Mass Inter Tred ikifanya usafi kila kona ndani ya ukumbi wa bunge na nje ya ukumbi wa jengo la bunge.

Madhari ya bustani za eneo hilo la vya bunge vizanaonekana katika hali ya kuvutia kutokana na kazi inayofanywa na kampuni hiyo ya usafi.

Mbali na hilo maofisa wa bunge nao walikuwa wakiendelea kupeana semina jinsi ya kuwapokea wabunge wateule na kuwafanyia usajili kutokana na kile kinachoadaiwa kwamba watumishi wengi wa bunge ni wageni.

Kwani kuna taarifa kuwa wafanyakazi wengi wenye uzoeefu wa shughuli hizo za ofisi za Bunge wamehamishiwa katika Ofisi za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa maofisa wa bunge ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji, amesema usajili wa wabunge wateule unatarajiwa kuanza leo na utaendelea hadi siku ya Jumapili.

“Kwa sasa kinachoendelea hapa ni maandalizi ya hali ya usafi wa mazingira na upangaji wa viti ndani ya bunge pamoja na huduma mbalimbali ambazo ndiyo zinaendelea kufanyiwa kazi ili ifikapo siku ya Jumanne Novemba 17, mwaka huu, wabunge hao wateule waapishwe,” amesema.

Aidha, MwanaHALISI Online pia lishuhudia ulinzi mkali ukiendelea kuimalishwa katika maeneo mbalimbali ya viwanja vya hivyo vya Bunge.

Askari wako makini katika kuhakikisha kwamba kila raia anayefika haka katika eneo hilo anapekuliwa kisha kujisajili wapi anakoelekea.

Kwa upande mwingine kuhusu sulala la utulivu, inaonekana bado mji huo Dodoma kuwa katika utulivu mkubwa huku wananchi waliyo wengi wakiendelea, shughuli zao na wakisubiri ugeni huo mkubwa.

Kuhusu wapambe

Wabunge wengi wateule wamesema kwamba siku ya kuanzia Jumapili watakuwa na wageni wengi ambao watafika bungeni kwa ajili ya kushuhudia jinsi wabunge wao wanavyoapishwa.

Mmoja wa wabunge wateule, kutoka katika jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka (CCM) amesema yeye anao wageni zaidi ya 20.

Naye Mbunge wa Viti Maalum, Conchester Rwamlaza amesema yeye ana wageni zaidi 30 ambao wataweza kufika katika maeneo hayo kwa lengo la kuhakikisha wanashuhudia jinsi anavyoapishwa.

Bei za vyakula

Kwa upande wa bei za vyakula katika mji wa Dodoma, zimepanda, jambo ambalo linaonekana kuwa tatizo kubwa kwa walaji.

Sababu kubwa ya kupanda kwa bei ni kutokana na ugeni wa wapambe wa wabunge wateule ambao wataambatana na wabunge hao.

Sababu nyingine ya kupanda kwa vyakula katika mkoa wa Dodoma, ni pamoja hali mbaya ya wakulima kushindwa kupata mazao ya kutosha.

Baadhi ya bidhaa zilizopanda ni viazi mviringo, unga wa sembe, sukari, mchele pamoja na nyanya.

Mwenyekiti wa soko la matunda na mbogambonga la Sabasaba, Athumani Makole amekiri bei ya bidhaa kupanda huku akieleza siri ya mfumuko huo wa bei hasa kwa upande wa viazi mviringo kutoka Sh.800 hadi kufikia 1800 unasababishwa na uzalishaji mdogo wa zao hilo .

“Sasa hivi ni msimu wa kilimo hivyo wakulima wa Kyera ampao ndipo tunapochukulia viazi mvilingo wanalima kidogo hali inayosababisha kutusambazia mzigo mchache na hivyo wafanyabiashara kujipangia bei wanayoitaka wao masokani,” amesema Makole.

Awali kilo ya viazi mviringo ilikuwa kati ya Sh. 800 hadi kufikia Sh 1,800, unga wa sembe kutoa Sh. 1,000 hadi 1,200, nyanya Sh. 3,000 hadi 6,500 na kwa upande wa nyama kutoka Sh. 6,000 hadi 7,500.

error: Content is protected !!