September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taslima:Ninatosha Uenyekiti CUF

Spread the love

 

TWAHA Issa Taslima, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF) amesema kutokana na uzoefu alio nao anastahili kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho na anatosha, anaandika Regina Mkonde.

Taslima ambaye kwa taaluma ni Mwanasheria ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akijibu swali la mwandishi wa habari lililohoji kuwa kama anavigezo na sifa za kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF Pro. Ibrahim Lipumba katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.  

“Chama chochote kikifika katika kipindi cha uchaguzi  huwa kina kipindi kigumu na ndicho kipindi nilichoingia kwenye nafasi ya uenyekiti wa kamati ya uongozi wa CUF Taifa.

Katika kipindi hicho nilipata uzoefu na kuona mambo ambayo yanahitajika kufanywa katika vipindi hivyo. amesema na kuongeza.

“Naweza nikasema kwamba ninatosha na ninaweza maana hata walionichagua na kuhudumu nafasi ya uenyekiti kwa kipindi cha miezi kumi tena kipindi kigumu hawajawahi kuniambia ondoka kutopkana na kushindwa kazi.”

Aidha, Taslima amesema kuwa wanachama wa CUF na wananchi kiujumla wanatakiwa kujua kwamba kauli aliyoitoa Lipumba hivi karibuni ya kutengua barua yake ya kujiuzulu aliyomwandikia Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad, haitazuia uchaguzi wa chama hicho kufanyika.

“Tulitaka tuweke mambo sawa kwa wananchi kwamba kauli ya Lipumba ya kutengua barua ya kujiuzulu kwake haimaanishi kwamba bado anashikilia wadhifa wa uenyekiti, bali kamati ya uongozi iko pale pale hadi mkutano mkuu wa kuchagua viongozi utakapofanyika,” amesema Taslima.

Amesema kauli inayotolewa na baadhi ya wananchama wa CUF ya kwamba hakuna mwanachama wa chama hicho mwenye uwezo wa kurithi na kuvaa viatu vya Lipumba si ya kweli na kwamba wako wanachama wenye uwezo huo na zaidi.

“Hao wanachama wanaosema kuwa Lipumba kwanza chama baadae na kwamba hakuna mwanachama atakayeweza vaa viatu vyake si wa kweli, chama hiki ni cha kila mtu na nafasi za uongozi zinastahili kugombaniwa na kila mtu,” amesisitiza

 

error: Content is protected !!