July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TASAF III yanufaisha 260,173

Nyumba ya kijijini

Spread the love

KAYA 260,173 zimenufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu (TASAF III) hadi kufikia Machi 2015, ambapo zaidi ya Sh. 48 bilioni zimehawilishiwa kwa masharti ya lishe, elimu na afya. Anaandika Danny Tibason … (endelea).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Dk. Mary Nagu ametoakauli hiyo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Fakharia Shomar Khamis (CCM), ambaye alitaka kujua ni kaya ngapi ambazo zimeweza kunufaika na mradi huo kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Pia mbunge huyo, alitaka kujua ni kaya ngapi ambazo tayari zimeweza kubadilika kimaisha baada ya kunufaika na mradi huo.

Dk. Nagu ameliambia Bunge kuwa, mradi huo unatekelezwa katika halmashauri 159 za Tanzania Bara pamoja na Unguja na Pemba, ambapo idadi ya walengwa wanaotarajiwa kufikiwa ni kaya maskini zaidi ya milioni moja.

Amesema kaya hizo zina takribani watu milioni saba na walengwa walitambuliwa kupitia mikutano ya vijiji na mitaa.

“Uhawilishaji fedha kwa kaya maskini ulianza rasmi Januari 2014, katika mamlaka za maeneo ya utekelezaji 40, kwenye vijiji, mitaa na Shehia 1,983. Kwenye mikoa ya Pwani, Morogoro, Mara, Ruvuma, Mbeya, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara, Katavi na Kigoma pamoja na Unguja na Pemba,”amesema.

Amefafanua kuwa, uhawilishaji ambao umeshafanyika katika maeneo kwa kiasi kikubwa umeshaanza kubadilisha maisha ya watu waliomo katika kaya hizo.

Kwa mujibu wa Dk. Nagu, kaya hizo zina uhakika wa kupata zaidi ya mlo mmoja kwa siku na pia kaya zenye watoto wanaokwenda shule wanatakiwa kuhudhuria masomo bila kukosa.

error: Content is protected !!