January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TAS walalamika kutengwa

Viongozi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) walipozungumza na Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

CHAMA cha Albino Tanzania (TAS), kimeilalamikia Serikali, kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa kutowashirikisha katika kupanga bajeti maalum kwa ajili ya kushughulikia saratani ya ngozi ambayo inaendelea kuwapukutisha. Anaandika Sarafina Lidwino (endelea).

Katibu Mkuu wa TAS, Ziyada Msembo, amewaambia waandishi wa habari kuwa, “licha ya kutoshirikishwa kwenye bajeti yetu lakini bado tuna matumaini kuwa mwaka huu, serikali kupitia Bunge la bajeti itatoa mwelekeo wa kushughulikia masuala ya Albino.”

Ziada ameongeza, “…tunatumaini pia Wizara ya Mambo ya Ndani na wizara nyingine zitatekeleza kauli ya Rais Jakaya Kikwete juu ya nia yake ya kukomesha mauaji ya Albino. Nasi tutaenda bungeni Juni 26 mwaka huu, kusikiliza mawasilisho yao.”

Kuhusu maadhimisho ya kitaifa ya siku ya Albino, ambayo yalikuwa yanafanyika kila Mei 4 ya kila mwaka, sasa yatakuwa yakifanyika Juni 13 kila mwaka.

Mabadiliki hayo yalifanyika baada ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo walipanga yatakuwa yakifanyika siku moja duniani kote.

Amebainisha kuwa, hapa nchini maadhimiaho hayo yalianzishwa na TAS, ambapo yalikuwa yakifanyika katika mikoa tofauti na kwamba mwaka huu, yatafanyika Mkoa wa Arusha.

“Hadi sasa tumeshawaandikia barua za mwaliko nchi tofauti zipatazo 20, hivyo runatarajia kuwa na wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi. Rais Kikwete ndiye atakuwa mgeni rasmi,” amesema Msembo.

error: Content is protected !!