Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko TARSI, Polisi yawapika wanafunzi usalama barabarani Dar
Habari Mchanganyiko

TARSI, Polisi yawapika wanafunzi usalama barabarani Dar

Spread the love

 

WAKATI Serikali ikipambana kupunguza vifo vitokanavyo na ajali barabarani Taasisi ya Tanzania Road Safety Initiatives (TARSI) imeunga mkono jitihada hizo kwa kutoa elimu ya usalama barabara kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) … (endelea)

Leo tarehe 25 Julai, 2022, Taasisi hiyo ikishirikiana na Jeshi la Polisi wilayani Kinondoni wamefika katika shule ya Sekondari ya Kambangwa wilayani humo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwapa elimu ya Usalama barabarani wanafunzi.

Akizungumza wakati wa utoji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa TARSI, Maliki Balongo, amewasihi wanafunzi kuzingatia elimu ya usalama barabarani kwa kuwa wao ni walengwa kwenye ujenzi wa taifa.

Balongo amesema kuwa Taasisi hiyo imezichagua shule za awali, msingi na sekondari kwa kuwa hivyo ndio vituo vya watunga sera, wanatekelezaji na wasimamiaji sheria wa baadae.

Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya hiyo ASP Notker amesema jeshi la polisi limewiwa kutoa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa shule mbalimbali kwa kuwa wao ni sehemu ya wathirika wa ajali za barabani.

Nokter amesema kuwa wanafunzi ni wabebaji na wasambazaji wa ujumbe kwa haraka kwa kuwa wepesi kukariri na kuwaelekeza wazazi wao na wenzao wakiwa michezoni “wanafunzi hawa ni wepesi kujifunza na kupitia wao watapeleka ujumbe kwa wazazi pamoja wanafunzi wenzao wakiwa michezoni.”

Amesema kuwa kundi hilo ni muhimu kwenye ujenzi wa jamii hususan taifa la kesho, “hatuwezi kujenga taifa lenye walemavu wengi au vifo vingi vitokanavyo na ajali za barabarani hivyo elimu hii itawasaidia kufahamu kwa umakini sheria.”

Hailaiti Justine Mwanafunzi wa shule hiyo akizungumza na MwanaHALISI ONLINE amesema kuwa amefurahi kufahamu alama za barabarani, na kwamba elimu hiyo itawasaidia wanafunzi kujiepusha na ajali za barabarani.

“Tumejifunza mengi kuhusu usalama barabarani na kwenye shule hii kuna wanafunzi wanaotoka sehemu tofauti na wenye kutumia barabara kwenda na kurejea nyumbani hivyo elimu hii itatusaidia kusalimisha maisha yetu barabarani” amesema Hailaiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!