Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko TARI kuwaondolea wakulima mbegu za zamani
Habari Mchanganyiko

TARI kuwaondolea wakulima mbegu za zamani

Baadhi ya mifuko ya mbegu bora za kisasa
Spread the love

TAASISI ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kitengo cha Uhawilishaji teknolojia na mahusiano ina mpango wa kuzalisha mbegu za aina mbalimbali kwa ajili ya kuwafikia wakulima na kuwaondoa katika matumizi ya mbegu za kizamani huku zikiwa hazina tija kwao. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Mkurugenzi Mkuu wa (TARI), Dk. Geofrey Mkamilo amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la ofisi ya TARI iliyopo kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere vya maonesho ya wakulima kanda ya mashariki 88 mkoani Morogoro.

Dk. Mkamilo amesema kuwa licha ya uwepo wa makampuni machache ambayo yanazalisha mbegu kwa idhini ya Serikali hapa nchini ikiwemo kampuni ya mbegu ASA lakini bado kumekuwa na upungufu mkubwa wa upatikanaji wa mbegu jambo inalofanya wakulima kuendelea kutumia mbegu za zamani na kushindwa kuzalisha kwa faida.

“Zipo mbegu zaidi ya aina 200 za mazao mbalimbali yakiwemo ya mizizi na mafuta ambazo kwa kiasi kikubwa hazizalishwi na ASA licha ya kuwa na kibali cha kuzalisha mbegu, kupitia kitengo hiki tutahakikisha tunazalisha mbegu zote ili mkulima asikose mbegu kwa maendeleo yake na Taifa kwa ujumla,” amesema Dk. Mkamilo.

Aidha Dk. Mkamilo amesema, katika kufikia na kutimiza azma ya Serikali ya Viwanda suala la kuboresha kilimo kwa kuanza na kuwepo kwa uzalishaji wa mbegu nyingi zenye ubora zenye uhakika kunahitajika ili kuendana na azma ya Serikali ya awamu ya 5.

Hivyo aliwaagiza watafiti waliopo kwenye vituo 16 vya Utafiti wa mazao mbalimbali nchini yakiwemo ya biashara watumie nafasi ya uhawilishaji waliyonayo kuhakikisha wakulima waliopo kwenye maeneo yanayowazunguka wanalima mazao hayo kwanza na baadae wayafikishe kwa wakulima wengine walio mbali.

“Hii itasaidia hata wakulima wengine kutoka maeneo ya mbali wanapofika kwenye maeneo jirani na vituo vyetu vya utafiti kuweza kupata elimu na ujifunza kabla ya kuanza kutumia utafiti na mbegu zinazozalishwa na vituo vyetu,” amesema Dk. Mkamilo.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Injinia Matwew Mtigumwe amewaagiza watafiti hao kuhakikisha wanazingatia kuwa Tafiti wanazozalisha zinamsaidia mkulima ili kupiga hatua kubwa ya mandeleo ya Kilimo hapa nchini.

Injinia Mtigumwe amesema kuwa maendeleo ya viwanda yanategemea kilimo ambapo Wizara ina program kubwa ya maendeleo ya kilimo ya miaka mitano kwa kuanza na mazao matano ili kuinua uchumi wa mkulima pamoja na Korosho Pamba, Chai na Tumbaku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!