
Philemon Ndesamburo enzi wa uhai wake
MBUNGE wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi, anaandika Mwandishi Wetu.
Basil Lema, Katibu wa Chadema, Mkoa wa Kilimanjaro, amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi juu ya kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe.
MwanaHALISI Online itaendelea kuwajulisha kuhusu msiba huo, endelea kuwa nasi.
More Stories
TANESCO yaghairi matengenezo mfumo wa LUKU
Dk. Mpango atoa somo Wimbo wa Taifa
Ruto: Machifu, watumishi ‘waliotekwa’ upinzani warejee kazini