August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzia: Mchoraji nembo ya Taifa afariki

Mzee Francis Maige alipokuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili

Spread the love

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imetoa taarifa za kifo cha Mzee Fransis Maige (86) aliyechora Nembo ya Taifa ya Uhuru na Umoja ambayo inatumika nchini hadi sasa, anaandika Hamisi Mguta.

Maige amefariki karika hospitali hiyo wakati akipatiwa matibabu ambapo awali alifikishwa katika hospitali ya Amana chini ya usimamizi wa viongozi wa serikali akiwemo Naibu wa ziri wa Afya Dk. Khamisi Kigwangala baada ya watu mbalimbali kulaumu serikali kwa kumuacha akiteseka na magonjwa huku akiishi kwa shida kutokana na umuhimu wake na mchango mkubwa katika Taifa.

Aminiel Aligaesha, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ua Umma katika hospitali ya Muhimbili amesema Maige alifikishwa hospitali ya Muhimbili siku ya Alhamis Mei 25 mwaka huu hapo akitokea hospitali ya amana lakini jana Mei 29 hali yake ikabadilika ghafla.

“Jana Mei 29 hali yake ilibadilika ghafla na madaktari wetu walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake lakini hawakufanikiwa,” amesema Aligaesha.

Mwili wa marehemu Maige umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri taratibu za mazishi kama itakavyowekezwa mamlaka husika.

error: Content is protected !!