Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17, (Serengeti Gilrs), imefanikiwa kutinga kwa mara ya kwanza kwenye fainali za kombe la dunia, zinazoandaliwa na shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), mara baada ya kuwaondosha timu ya taifa ya Cameroon. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wasichana hao wamefuzu kwa jumla ya mabao 5-1, katika michezo yote miwili, ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Cameroon majuma mawili yaliyopita waliondoka na ushindi wa mabao 4-1.

Bao pekee la Tanzania kwenye mchezo huo liliwekwa kambani na Neema Paul Kinega, na kuandikisha historia hiyo ya kipekee.

Faina hizo zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini India, aambpo Tanzania imeungana na timu za Taifa za Nigeria pamoja na Morocco ambao wameshakwisha kata tiketi, ndani ya bara la Afrika.

Mara baada ya ushindi huo, klabu mbalimbali sambamba na wadau wa mchezo huo, walitoa salamu za kuwapongeza wasichana hao kwa kuweka rejodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania, kufuzu kwa fainali hizo zinazoandaliwa na FIFA.

Katika harakazi za kutafuta tiketi hiyo, Serengeti Gilrs kwa nyakati zote, chini ya kocha wao Bakari Shime walichezea michezo yao ya nyumbani visiwani Zanzibar kwenye dimba la Amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *