March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania yashinda tuzo ya utalii Urusi

Serengeti

Spread the love

NCHI ya Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa mwaka 2018 nchini Urusi, katika kipengele cha eneo bora zaidi la utalii duniani (The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tuzo hiyo ilipokelewa jana tarehe 21 Novemba 2018 na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi kutoka kutoka Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi.

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii.

Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo katika kundi la eneo bora la utalii duniani.

error: Content is protected !!