March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania yashinda tuzo ya kimataifa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Spread the love

TANZANIA imetunukiwa tuzo ya Kimataifa ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambikiza. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tuzo hiyo alikabidhiwa jana tarehe 27 Septemba 2018 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt.Soumya Swaminatha Mjini New York nchini Marekani.

Tuzo hiyo imetolewa na kikosi kazi Maalumu cha Umoja wa Mataifa (UN) mahsusi kwa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs- UNIATF).

Tanzania imepewa tuzo hiyo kama sehemu ya kutambulika kwa juhudi zake kupitia Wizara ya Afya katika kupambana dhidi ya magonjwa hayo ikiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na saratani.

error: Content is protected !!