October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania yapokea chanjo ya corona kutoka China

Spread the love

 

TANZANIA leo Ijumaa, tarehe 8 Oktoba 2021, imepokea dozi 576,558 za chanjo dhidi ya ugonjwa unaoambukizwa na virusi vya korona (UVIKO-19) aina ya Sinopharm kutoka China. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema, “dozi hizo zimeletwa nchini chini ya mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uitwao Covax Facility na ni sehemu ya Dozi 1,065,600. Dozi nyingine 489,042.”

Tayari Tanzania ilikwisha kupokea dozi milioni moja aina ya Johnson & Johnson ‘JJ’ kutoka Marekani.

Chanjo hiyo JJ ndiyo ambayo tarehe 28 Julai 2021, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliizindua Ikulu ya Dar es Salaam kwa yeye mwenyewe kuchanjwa na inaendelea kuchanjwa kwa wananchi walio tayari.

error: Content is protected !!