SERIKALI ya Tanzania, imeongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa na George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani, jijini Dodoma jana Jumapili, tarehe 27 Juni 2021.
Amesema, juhudi hizo zinawekwa ili kuokoa vijana ambao ni nguvu kazi kwa Taifa ambapo waziri huyo amekumbusha waraibu wa dawa hizo wapewe mitaji pale watakapoondoka kwenye matumizi hayo.

Kwenye kilele hicho, Simbachawene ametoa maagizo kadhaa katika hatua za kupambana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kuelimisha wanahabari ambao huwasiliana na wananchi kupitia maandiko na vipindi vya redio na televisheni.
Pia, ameshauru wizara ya elimu, sayansi na teknolonia kuboresha mitaala kuwezesha vijana kupata elimu juu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya.
Maagizo mengine ya serikali ni kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu na viongozi wa dini kukemea matumizi ya dawa za kulevya.
Waziri Simbachawene amesema, kuna matumizi makubwa ya dawa za kulevya na kwamba matumizi ya bangi yakiongoza kwa kuwa na watumiaji wengi ikifuatiwa na heroin na cocaine ambazo huingia kutoka nje ya nchi.
Leave a comment