Thursday , 2 February 2023
Home Kitengo Michezo Tanzania yampa uraia Denis Kibu, rasmi Simba
MichezoTangulizi

Tanzania yampa uraia Denis Kibu, rasmi Simba

Chibu Denis (kushoto) akiwa katika kikosi cha Taifa Stars. Kulia ni John Bocco
Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene, amehitimisha sakata la uraia wa Kibu Denis Prosper kwa kutangaza kumpa uraia mchezaji huyo wa Simba. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).

Simbachawene ametumia mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), kumpa uraia Kibu.

Uamuzi huo umetangazwa usiku wa Jumamosi tarehe 2 Oktoba 2021 kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter wa wizara hiyo uliyoweka picha ya Kibu na maneno yaliyosomeka;

“Mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi lililoletwa kwake na TFF, amempa URAIA wa Tanzania Mchezaji wa Mpira wa Miguu, Kibu Denis Prosper, Sept. 30, 2021.”

Waziri Simbachawene ametangaza uamuzi huo ikiwa imepita siku moja tangu, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuibuka na kumtaka, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati suala hilo akidai linatia aibu Taifa.

Mbali na Majaliwa, Zitto aliwatupia mzigo Waziri Simbachawene na Innocent Bashungwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo akisema, wakiamua wanaweza kuhitimisha suala hilo ndani ya siku moja.

Zitto aliibuka kuzungumzia suala hilo alipofanya mahojiano maalumu na MwanaHALISI TV na MwanaHALISI Online akishangazwa na uamuzi wa Serikali kushikilia hati ya kusafiria ya Kibu ambaye amesajiliwa Simba msimu huu akitokea Mbeya City.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) alisema, ilikuwaje Kibu akacheza Mbeya City, timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars “hakuulizwa uraia, ila amesajiliwa tu Simba anaulizwa uraia.”

Kibu anayevalia jezi namba 38 aliyopewa baada ya kusajiliwa Simba, aliicheza Taifa Stars kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi, tarehe 13 Julai 2021, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Stars kuibuka na ushindi wa 2-0.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani

Kwenye mchezo huo, Kibu anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alionesha kiwango kinachoridhisha na kuwezesha ushindi huo na baadaye akizungumza na waandishi wa habari alisema “nashukuru sana kwa mara ya kwanza kuichezea timu yangu ya Stars. Wazidi kunipa moyo kwani safari bado ndefu.”

Baada ya uamuzi huo wa Serikali, Zitto ameandika kwenye Instagram yake akipongeza uamuzi huo akisema “nazishukuru na kuzipongeza mamlaka za uraia.”

6 Comments

 • Habar yenu haijajitosheleza ! Hamjaweka waz kua alikua na uraia wa nchi gan ? Mmewaweka njia panda wasomaj wa taarifa yenu .

 • Kwa kweli kuna ukakasi ndani yake maana raia hawezi kuombewa uraia kwa waziri husika.

 • Zingatieni weledi ktk kutoa taarifa. Taarifa haipo kamili kwa sababu hamjasema alikua na uraia wa wapi kabla. Huenda hamjatafiti kabisa kuhusu habari hii. Naweza kusema hakuna habari hapo. Yote mliyoandika tayari tunayajua kabla hata hamjaandika. Tunaomba mfanyie kazi changamoto hiyo.

 • UADISHI WA HABARI WA UKANJANJA:
  1.Alikkuwa Raia wa Nchi ngani
  2.Nani wanalalamika
  3. Je kuna ufafanuzi wowote kwa waliokuwa wamemuajiri bila vibari
  4Kama Mwandishi si vibaya ungekuja na Hitimisho ukijikita kwenye reason leant

 • UADISHI WA HABARI WA UKANJANJA:
  1.Alikkuwa Raia wa Nchi ngani
  2.Nani wanalalamika
  3. Je kuna ufafanuzi wowote kwa waliokuwa wamemuajiri bila vibari
  4Kama Mwandishi si vibaya ungekuja na Hitimisho ukijikita kwenye reason leant

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bilioni 213 za miradi ya DMDP zaistawisha Temeke

Spread the loveJUMLA ya Sh bilioni 213 zimetumika kuboresha sekta ya afya,...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aibuka na bei za vyakula, “Njaa inadhalilisha nchi”

Spread the loveMBUNGE wa kuteuliwa na Rais, Dk. Bashiru Ally, ameitaka Serikali...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ahoji fedha za Plea-Bargaining

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ameitaka Tume ya kuangalia namna...

error: Content is protected !!