December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania yajinasibu na BRN

Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa miradi (PDB), Omari Issa

Spread the love

MIAKA  miwili tangu utekelezaji wa mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), uanze hapa nchini kwa utekelezaji  na kuonyesha matokeo mazuri katika kuboresha huduma za jamii. Anaandika Faki Sosi, DSJ … (endelea).

Aidha, imejinasibu kuwa kutokana na kufanikiwa kwake  Jumuiya za kimataifa na nchi nyingine kadhaa zimetamani kuja nchini kujifunza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa miradi (PDB), Omari Issa jijini Dar es salaam.

Issa amesema kuwa Tanzania imepata matokeo makubwa katika sekta mbali mbali na kuongeza ufanisi katika utendaji na utekelezaji wa miradi ili kuharakisha upatikanaji wa huduma za umma

“Sisi tumejifunza kutoka mfumo wa Malaysia uitwao Matokeo Makubwa ya Haraka lakini tulionganisha na vipao mbele vya mazingira yetu, kwani mahitaji yetu ni tofauti na kwao,” amesema.  

Amesema kuwa PDB ipo tayari kutoa uzoefu wake kuhusu utekelezaji wa BRN kwa nchi za jumuiya ya madola na changamoto ya utekelezaji upo katika nchi nyingi.

Hivyo ni muhimu katika kujifunza kwa nchi nyingine kutokana na udhoefu waliopata ikiwa baadhi ya nchi wametuma watendaji wao kuja kujifunza

Amesema  kuwa utekelezaji wa ufanisi na matokeo makubwa umeonekana katika sekta ya nishati kwa asilimia 10, maji watanzania milioni 2.36 wamepata maji safi na upande wa usafirishaji asilimia 18 ikiwa sekta elimu, kilimo na sekta nyengine

error: Content is protected !!