KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa wito kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza katika zao la korosho, kushiriki katika jukwaa linalotarajiwa kufanyika kuanzia Julai 12-13, 2019 mkoani Mtwara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Jana tarehe 21 Juni 2019 TIC kilitoa mwaliko kwa wawekezaji watakaohitaji kushiriki katika jukwaa la korosho, ambapo Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Kwa mujibu wa mwaliko huo, jukwaa la Korosho linalenga kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya Tanzania na wawekezaji wa ndani, katika uanzishwaji wa viwanda vya uongezaji thamani zao la korosho hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Vile vile, katika jukwaa hilo washiriki watapata fursa ya kusikia mada kutoka kwa maafisa wakuu wa serikali ikiwemo Rais Magufuli, pamoja na kufanya mazungumzo na majadiliano na wataalamu wa zao hilo pamoja.
Fursa zilizotangazwa katika uwekezaji wa korosho, ni pamoja viwanda vya uongezaji thamani korosho ghafi, uanzishwaji wa mashamba makubwa ya korosho, biashara ya usambazaji wa vifaa na vipuri vya mitambao ya mashine za kuongeza thamani korosho.
Leave a comment