Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Tanzania yaiomba Benki ya Dunia dola 100 Mil.
Habari Mchanganyiko

Tanzania yaiomba Benki ya Dunia dola 100 Mil.

Bonde la Mto Msimbazi
Spread the love

SERIKALI imeiomba Benki ya Dunia (W.B)  msaada wa fedha kiasi cha dola 100 milioni kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa bonde la mto Msimbazi jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ombi hilo leo tarehe 25 Februari 2019 jijini Dar es Salaam na Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI wakati akizungumza na maofisa wa W.B.

Jafo ameeleza kuwa, ni muhimu bonde hilo kufanyiwa marekebisho kutokana kwamba limekuwa chanzo cha vifo vya baadhi ya watu na uharibifu wa mali kwa sababu ya mafuriko yanayotokea wakati wa msimu wa mvua.

“Dola milioni 100 zinahitajika kukamilisha mradi wa kuboresha bonde hilo, ni matumaini yangu Benki ya Dunia mtashirikiana nasi kama am,bavyo tunashirikiana katika miradi mingine ya maendeleo,” amesema Jafo.

Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Benki ya Dunia wako nchini kwa muda wa siku mbili kuanzia leo hadi kesho tarehe 26 Februari 2019 kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!