Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania yaanza kupata kibano cha kimataifa
Habari za SiasaTangulizi

Tanzania yaanza kupata kibano cha kimataifa

Spread the love

KIBINYO kinachotokana na hatua ya serikali kugandamiza demokrasia nchini, kimeanza kuutafuna utawala wa sasa. Anaripoti Mwandishi Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa kutoka mataifa kadhaa ya Marekani na Ulaya zinasema, karibu mataifa yote ya maeneo hayo, ikiwamo Sweden, yanaitilia shaka amani ya Tanzania na kupoteza sifa ya kuwa baba wa demokrasia Afrika, tofauti na ilivyokuwa miaka sita iliyopita.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Finland na Denmark, Dk. Willibroad Slaa amesema, hatua ya baadhi ya watu kuituhumu serikali ya Rais Magufuli, kukandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa kutoa maoni, “kunawapa shida mabalozi kuitetea nchi huko walipo.”

“Vitendo hivyo vinawakatisha tamaa wahisani wanaotaka kuisaidia Tanzania. Wahisani wanaogopa kuleta fedha nchini na kwa kweli, hali yetu kisiasa kwenye mataifa ya nje, siyo nzuri,” ameeleza.  

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho taasisi kadhaa za ndani ya nchi, vikiwamo vyama vya siasa na mashirika ya madhehebu ya kidini, wakiituhumu serikali “kukandamiza uhuru wa wananchi wa kujieleza na kutoa maoni.”

Katika maelezo yake ambayo aliyatoa kwenye mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Star TV, Dk. Slaa amesema,  watalii zaidi ya 100 kutoka Sweden wameahirisha safari ya kuja nchini  kwa ajili ya kutalii.

Alimtuhumu kiongozi mmoja, ambaye hakumtaja jina kwa kusema, “…kauli za kiongozi mmoja, zimesababiha madhara makubwa kwa nchi.” 

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Star tv. Dk. Slaa ambaye aliwahi kuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema), alitoa kauli hiyo, wakati wa ziara ya mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali duniani walipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR eneo la Soga, mkoani Pwani.

Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi kadhaa duniani, wapo katika ziara ya kutembelea na kuijonea utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano kwa fedha za ndani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!