Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Tanzania ya kidijitali: Kuwekeza kwa vijana ni kuwekeza katika mustakabali sahihi
ElimuMakala & Uchambuzi

Tanzania ya kidijitali: Kuwekeza kwa vijana ni kuwekeza katika mustakabali sahihi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya TEHAMA yaliyoandaliwa na kampuni ya HUAWEI
Spread the love

VIJANA wa Tanzania ni rasilimali muhimu zaidi ambayo nchi inatakiwa kuwa nayo katika siku za usoni. Umuhimu wa vijana unatokana na ukweli kwamba nguvu, maarifa na ujuzi wao ni kiini cha mafanikio ya nchi kwa wakati uliopo na hata siku zijazo.

Katika kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na kesho thabiti, hakuna budi kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa kiini cha mipango ya maendeleo. Kukamilisha hili mambo mengi yanahitaji kuzingatiwa ikiwemo ujengewaji wa ujuzi husika kulingana na dira na mahitaji ya nchi. Changamoto zinazowakabili hazipaswi kufumbiwa macho pia.

Kwa kuwa teknolojia inabadilika kwa haraka, kuna haja kubwa pia ya kuhakikisha kuwa kama taifa tunaendana na mabadiliko hayo hasa katika maeneo ya maarifa na ujuzi. Kuendana na kasi hiyo uanzishwaji wa programu mbalimbali za mafunzo kwa vijana ni jambo linalostahili kipaumbele hasa wakati huu ambao nchi inajidhatiti kuelekea uchumi wa kijiditali.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya TEHAMA yaliyoandaliwa na kampuni ya HUAWEI

Mpango wa mafunzo yenye lengo la ujengaji na ukuzaji wa maarifa na ujuzi ni vyema ukahusianishwa na mfumo rasmi wa elimu na kwa kuzingatia ngazi zote kuanzia elimu ya msingi hadi ngazi ya elimu ya juu. Ni katika kuchukua hatua iyo ndipo hasa kama taifa tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuwa na wataalum wabobezi katika sekta ya TEHAMA siku za usoni.

Tumeshuhudia ili kukidhi mahitaji ya maarifa na ujuzi katika sekta ya TEHAMA kulingana na mabadiliko ya kasi ya sekta hiyo, serikali imekuja na mipango mbalimbali katika ngazi mbalimbali za elimu. Kwa kuangazia hii inajumuisha Programu ya kujenga shule moja ya Sayansi kwaajili ya wasichana kwa kila Mkoa. Mipango ya namna hii inaonesha dhamira njema ya serikali katika kuwainua wasichana kwenye sekta ya TEHAMA na hatimaye kuwa na wataalamu wa kutosha ambao watakuwa madereva wazuri wa uchumi wa kidijitali.

Pamoja na jitahada hizo za serikali bado jitihada zaidi zinahitajika ili kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na rasilimali watu inayoendana na hitaji la soko la ajira katika sekta ya TEHAMA nchini Tanzania na Duniani kwa ujumla.

Uharaka wa kukuza vipaji zaidi ni jambo la kupewa kipaumbele kikubwa kwa sasa. Kulingana na ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia, ambayo inakadiria kuwa ajira milioni 230 katika Kusini mwa Jangwa la Sahara itahitaji ujuzi wa kidijitali ifikapo mwaka 2030. kama hatutachukua hatua sasa Tanzania na Afrika itabakia katika kundi la nguvu kazi isiyovutia na yenye uwezo duni wa kukidhi vigezo vya soko la ajira la kisasa.

Kwa kuzingatia hilo, ni wakati muafaka sasa wa wadau wa sekta ya elimu pamoja na sekta ya TEHAMA kuangalia namna sahihi ya kuzalisha vijana kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira kwa nyakati zijazo.

Miongoni mwa mambo ambayo wadau wa sekta hii wanapasa kutazama ni uanzishaji wa mpango wa kimkakati wa programu mbalimbali katika taasisi za elimu ambazo zitalenga kuwajengea uwezo, kuwaongezea maarifa na ujuzi wanafunzi wa Tanzania.

Kupitia programu hizo, vyuo na vyuo vikuu havina budi kufanya marekebisho ya maudhui ya jadi ya mitaala na badala yake vijikite zaidi katika ufundishaji wa teknolojia za kisasa zaidi. Mambo ya kuzingatia ni kuhakikisha kuwa kozi zinaendana na wakati, kuzingatia kuwa vifaa vya kufundishia vinalingana na mazingira ya sasa ya soko na hivyo kuwasaidia wanafunzi kuwafanya wawe na sifa za kuajirika.

Mfano, Mwaka 2019 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiliingia katika ushirikiano na Kampuni ya Teknolojia ya Huawei. Ushirikiano huu umejikita katika ukuzaji wa vipaji vya vijana wa kitanzania wanaosoma kada ya TEHAMA.

Kupitia ushirikiano huo, Huawei inafanya kazi na wahadhiri ili kuendeleza kozi kwa pamoja kulingana na uelewa wa Huawei wa sekta ya TEHAMA, mkusanyiko wa kiufundi, pamoja na uzoefu.

Kutokana na Programu hiyo wanafunzi hupata fursa ya kujifunza na kuboresha kwa kiasi kikubwa ujuzi na maarifa yao.

Hivyo basi, kwa kuwa na msururu wa ushirikiano wa namna hii na makampuni vinara katika sekta ya TEHAMA, kama taifa tunaweza kutengeneza vijana wa kutosha ambao watakidhi mahitaji ya soko la TEHAMA na mwisho kusaidia katika maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

Makala imeandaliwa na Mhadhiri Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Dk. Dossa Massa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 28 watumishi UDSM yaliwa na nzige, madumadu

Spread the loveGEORGE Francis anasikitika; anatembea akiwa na mawazo mengi, hajui la...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nimekumbuka Samia wa miaka 3 iliyopita

Spread the loveWAKATI naandaa makala ya safu hii wiki hii, nimejikuta nakumbuka...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hakuna fedha za Rais

Spread the loveKUNA mambo machache mazuri ya kujifunza kutoka kwa Margaret Thatcher,...

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

error: Content is protected !!