Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa utalii duniani
Habari Mchanganyiko

Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa utalii duniani

Spread the love

 

TANZANIA imesaini rasmi mkataba wa kukubali kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkubwa wa Utalii wa 65 wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani (UNWTO) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 5 hadi 7 mwaka huu Jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amesaini mkataba huo mbele ya Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvil, Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Madrid nchini Hispania.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri wote wa Utalii wa Bara la Afrika pamoja, Wabobezi wa kutangaza utalii na Wataalamu wa masuala ya utalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza mara baada ya hafla ya utiaji saini, Waziri Ndumbaro amesema mkutano huo ni fursa kwa Wadau wa utalii nchini Tanzania kujifunza na kubadilishana uzoefu mkubwa wa kuendesha Sekta ya Utalii hususani katika kipindi hiki ambacho sekta ya utalii imeanza kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO 19.

“Tumepewa heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa mkutano huu ambapo naamini utafungua milango ya vivutio vyetu vya utalii kujulikana Duniani kote” amesema Dkt.Ndumbaro.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvil amesema ataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika masuala ya utalii huku akiahidi kuipa kipaumbele Tanzania katika miradi mingi inayofadhiliwa na Shirika hilo.

“Nimekuwa nikipata ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania kupitia Waziri Dk. Ndumbaro, utiaji saini wa leo wa kuwa Mwenyeji wa mkutano huu ni mwanzo tu wa kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika masuala ya utalii” amesisitiza Katibu Mkuu huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!