Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania kuvuna matrilioni mradi bomba la mafuta
Habari za Siasa

Tanzania kuvuna matrilioni mradi bomba la mafuta

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inatarajia kuvuna matrilioni ya fedha, katika Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unaotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali hiyo na ya Uganda, kwa kushirkiana na wawekezaji. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tayari Serikali ya Tanzania na Uganda zimetia saini mikataba ya utekelezwa mradi huo kuanzia Hoima-Uganda hadi Tanga-Tanzania, ambapo leo Alhamisi, tarehe 20 Mei 2021, ilikuwa zamu ya Tanzania kusaini mkataba hodhi kati yake na wawekezaji wa EACOP, shughuli iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Shughuli hiyo, imeshuhudiwa na Marais wa nchi hizo, Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda. Ambao kwa pamoja walitoa tamko la kufunguliwa rasmi kwa shughuli za ujenzi wa bomba hilo.

Katika mradi huo, Serikali ya Tanzania na Uganda kila mmoja anamiliki asilimia 15 ya hisa (jumla asilimia 30), huku Kampuni ya Total ya Ufaransa ikimiliki asilimia 62 wakati Kampuni ya Uchimbaji Mafuta ya China (CNOOC) ikimiliki asilimia nane.

Nicolas Terraz, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Africa, amesema katika uwekezaji huo, Serikali ya Tanzania itapata Dola za Marekani 4 Bilioni (Sh. 9.27 trilioni).

“Matokeo ya kusainiwa mkataba huu, yatajenga msingi imara wa kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja, kutoka nje wenye thamani ya Dola 10 Bil. Ambapo utafanyika Uganda na Tanzania. Jumla ya uwekezaji wenye thamani ya Dola 4 Bil, utakwenda Tanzania,” amesema Terraz.

Naye Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk. Medard Kalemani, amesema mradi wa bomba hilo litakalotoa mafuta kuanzia Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania, utaingizia matrilioni ya fedha nchi.

Akizungumzia mradi huo, Dk. Kalemani amesema, katika hatua ya ujenzi wake, Serikali ya Tanzania, itapata asilimia 60 ya mapato yake, huku Uganda ikipata asilimia 40.

“Manufaa ya kwanza, mgawanyo wa mapato yatakayopatikana kutokana na uendeshaji shughuli za ujenzi haidi kukamilika kwa bomba na kuanza kuata faida. Nchi itapa asilimia 60 ya mapato yote ya bomba na Uganda 40,” amesema Dk. Kalemani.

Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati

Amesema asilimia 80 ya sehemu ya bomba hilo iko Tanzania, na 20 Uganda.

Faida nyingine ambayo Tanzania itapata mapato ya kikodi kiasi cha Dola 290 milioni (Sh. 672.36 Bil.), katika kipindi cha miaka 25 ya uhai wa mradi huo.

Hali kadhalika, Kampuni ya EACOP italipa kwa Serikali Dola 59 Mil. (136.79), kwa ajili ya kodi ya ardhi. Pamoja na Dola 73 Mil. (169.25), kwa ajili ya kutumia Bandari ya Tanga.

“Mengine kutakuwa na mapato ya kikodi, katika miaka 25 ya uhai wa mradi, nchi yetu itapata Dola 290 milioni, kwa kodi za moja kwa moja. lakini pia kwa sababu ardhi itatumiwa na Kampuni ya EACOP, kampuni zitakazoshiriki kujenga itakayoshiriki kuujenga italipa mapato kwa serikali kwa kutumia ardhi Dola 59 Mil.,” amesema Dk. Kalemani.

Amesema “kwa ajili ya kutumia bandari kuvusha mafuta katika ushirikiano wa nchi mbili, bado nchi itapa mapato Dola 73 Mil.”

Hayati Dk. John Magufuli na Rais Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakishuhudia mawaziri wa Nishati wa nchi zao (Mary Goretti
Kitutu-Uganda na Dkt.Medard Kalemani-Tanzania) wakitia saini
mkataba wa kuanza mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka
Hoima (Uganda)hadi Tanga leo

Mbali na faida hizo, Dk. Kalemani amesema, mradi huo utaongeza fedha za kigeni kwa asilimia 55, utatoa ajira zaidi ya 10,000 wakati wa ujenzi na 1,500 katika utekelezwaji wake.

Dk. Kalemani amesema mradi huo utapita katika vitongoji 527 kwenye wilaya 24 katika mikoa nane, Kagera, Geita, Tabora, Dodoma, Singida, Manyara na Tanga.

Mradi huo unatarajiwa kuanza rasmi mwaka 2024, baada ya ujenzi wake kukamilika.

Amesema ujenzi wa bomba hilo, vituo nane vitajengwa katika nchi zote (Uganda 2, Tanzania 6), na kwamba kwa upande wa Tanzania, vituo vinne vitakuwa vya kusukuma mafuta na viwili vitakavyojengwa mikoa ya Singida na Tanga, vitakuwa kwa ajili ya kupunguza spidi ya uingiaji mafuta hayo.

Pia, vituo 29 vya kulainishia vyuma vitajengwa katika nchi hizo (22 Tanzania na 7 Uganda). Pamoja na vituyo vya kufungia valvu 76 (53 Tanzania na 23 Uganda).

Hali kadhalika, Dk. Kalemani amesema matanki matano ya kuhifadhia mafuta yatajengwa katika Bandari ya Tabga, ambayo yana uwezo wa kuhifadhi lita 2.5 Mil. za mafuta.

Dk. Kalemani amesema miundombinu hiyo itainufaisha Tanzania siku zijazo, kwani ina dalili za kuvumbua mafuta katika Mikoa ya Singita, Tabora na Simiyu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!