June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania kushiriki maonyesho Italia

Uwanja wa maonesho ya Saba Saba

Spread the love

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), imesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 149 zitakazoshiriki maonyesho makubwa ya Dunia ya Expo Milan 2015 nchini Italia. Anaripoti Sarafina Lidwino (endelea).

Maonyesho hayo yatafanyika Mei 1,-31 Oktoba mwaka huu, na kubeba kauli mbiu isemayo “Kulisha Dunia Nguvu ya Uhai”.

Akizungumzia maonyesho hayo, Mkurugenzi mkuu wa TANTRADE, Jaquceline Maleko amesema, yamelenga katika sekta ya chakula, ambapo vyakula, mbinu na mikakati ya kuongeza na kuboresha aina za vyakula na mazao ya vyakula.

Amesema Tanzania itashiriki katika kundi la viungo, ambapo watapata fursa ya kuonyesha viungo mbalimbali kama chai, kahawa, korosho na mafuta yatokanayo na viungo.

Pia, wataonyesha utamaduni wa kitanzania unaoendana na chakula na namna ya viungo vya chakula vinavyoandaliwa kwa mapishi mbalimbali ya kitanzania.

“Ndani ya maonyesho hayo, fursa za biashara, uwekezaji na utalii zitaelezwa ikiwa ni pamoja ma vivutio mbalimbali kama, Mlima Kilimanjaro, fukwe za Zanzibar na hifadhi za Serengeti na Ngorongoro,” amesema Maleko.

Kuhusu namna ya kuondoka, amesema kwa mtanzania yoyote atakaependa kushiriki, anatakiwa kuchangia dola zisizopungua 1000, ambapo atapata tiketi, malazi na chakula kwa siku zote atakazo kuwa huko.

“Mshiriki anaweza kuchagua mwezi anaotaka kushiriki kati ya Mei-Oktoba. Tumejiwekea lengo la Watanzania wapatao 500 kutembelea maonyesho hayo kwa kipindi tofauti, hivyo nichukue fursa hii kuwaomba wafanyabiasha na mtu yoyote anaependa kujifunza aende,”amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo na biashara za nje, Anna Bulondo amesema, maandalizi ya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yamepangwa kufanyika tarehe 28 Juni hadi Julai mwaka huu.

Bulondo amesema ugawaji wa nafasi kwenye mabanda unaendelea, asilimia 85 ya mabanda yamechukuliwa. Amesema nchi 24 zitashiriki na makampuni 18 kutoka nje.

error: Content is protected !!